Liverpool kumsainisha mkataba nyota huyu.
Baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi zikimhusisha na kuwa mbioni kuihama
klabu yake , Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling
anatarajiwa kutia saini mkataba mpya utakaomfanya aendelee kubaki na
klabu hiyo kwa miaka mitano zaidi .
Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka magazetini nchini England asubuhi ya
leo (jumapili) , Sterling atatia saini mkataba huo ambao utamuingizia
mshahara wa paundi 100,000 kwa mwezi akiwa amepandishiwa mshahara kutoka
paundi 60,000.
Hatua hii inakuja siku chache baada ya klabu ya Liverpool kutangaza
kuwa nahodha wake wa muda mrefu Steven Gerard ataondoka klabu hapo
mwishoni mwa msimu huu huku ripoti zikisema kuwa atakwenda Marekani .
Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi zikimhusisha Sterling na kujiunga
na klabu bingwa ya Ulaya Real Madrid na taarifa za Sterling kusaini
mkataba mpya zitakuwa nzuri kwa mashabiki wa Liverpool katika kipindi
hiki ambacho klabu hiyo itampoteza Gerard .Sterling atasaini mkataba huo mpya mwishoni mwa mwezi huu wakati ambapo
mazungumzo na uongozi wa Liverpool yatakpokuwa yamekamilika na
kutangazwa rasmi .
No comments:
Post a Comment
paulmkale