Binti wa miaka 12 kutoka Nigeria kwenye rekodi kubwa za Kimataifa
Unapokuwa karibu na mtoto wako na
kumfuatilia ni rahisi kujua kipaji chake na kukiendeleza ingawa ni
wazazi wachache wanaoweza kufanya hivyo, msichana kutoka Nigeria ambaye
anasoma Marekani anakuwa msichana mdogo aliyeweza kuvunja rekodi kadhaa
kubwa duniani.
Zuriel Oduwole, umri wake ni miaka 12, ameweka historia nyingine baada ya documentary yake ya ‘A Promising Africa’ kuwa documentary ya binti mdogo zaidi duniani kuonyeshwa katika majumba makubwa ya cinema.
Jarida la Forbes lilimtaja kuwa
msichana mdogo mwenye asili ya Afrika ambaye ni miongoni mwa watu 100
mashuhuri wenye ushawishi zaidi Afrika waliotajwa kwa mwaka 2013
wakiwemo Marais watatu, pia akawa na rekodi ya kuwa mtu mdogo zaidi
dunia kuandikwa historia yake katika Jarida la Forbes.
Documentary hiyo itaonyeshwa London, Januari mwaka huu na baadaye itaanza kuuzwa.
No comments:
Post a Comment
paulmkale