Director yupi wa Bongo ambaye Kevin Bosco wa Kenya anamvutia yuko hapo chini

Mara nyingi imezoeleka kwa mashabiki kushindanisha vitu kwa mfano labda msanii fulani na msanii fulani ambapo wao baadae huwa wanakua na majibu ambayo hayana uhakika.

Kevin Bosco Jr ni jamaa kutoka Kenya ambaye kashiriki video nyingi sana za Kitanzania,kama umechek video za Ney hivi karibuni kama ile ya Mr Nay na hii ya Akadumba zote katengeneza yeye.

Pia kaongoza video ya AY ile ‘Ahsante’ video za Mwana FA ya ‘Mfalme’ na hii ya ‘Kiboko Yangu’, amekubali kutuambia muongozaji wa Bongo ambaye anavutiwa zaidi na kazi zake.

HansCana inaweza kuwa jina jipya kwako lakini kwenye ulimwengu huu wa video tayari  kashiriki video kadhaa za Bongo Fleva, huyu ndiye Director aliyetajwa na Director Kevin kuwa yuko vizuri na anazielewa video anazoongoza yeye.

Producer huyo HansCana amefanya video za Navy Kenzo, ‘Mama’ ya Y Tony, ‘Morare’ ya G Nako na kuna baadhi ambazo hazijatoka ikiwepo Vitamin Music ya Belle 9.

Hanscana ni muongozaji ninayemwangalia… anajua anachofanya kwa sababu nimeangalia video zake nampatia asilimia 90, anajua kuchagua location, story line inaenda yaani hata kama mtu kiziwi anaweza kuelewa pia hachomi picha‘ –Director Kevin Bosco Jr.

No comments:

Post a Comment

paulmkale