Zilianza
kwa kusikika taarifa kwa chinichini ila leo taarifa ikatoka mara baada
ya kusambaa zaidi kwa watu na mitandao ya kijamii habari kuwahusu wawili
hawa wanao sikika nchini.
MKALI
wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu ‘Wema’,
amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki
wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, kwa kumtapeli kiasi cha Sh
milioni 10
Kwa
mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili,
Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay akidai kuwa
alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa makubaliano ya kazi na
kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume makubaliano yao.
Muhusika
mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu wanamtupia lawama
kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai kuwa amelazimika kufanya
hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia dhamana na taasisi Focus Vicoba
kuchukua fedha hizo.
“Naona
watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi Diamond, pasipo
kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali ni mkopo ambao niliingia
dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo ya Vicoba.
“Kupitia
mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia
Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa
atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema
Wema.
Mrembo
huyo alieleza muda waliiopeana ahadi ya kurudisha fedha hizo umepita na
Diamond haoneshi dalili ya kuzirejesha wakati wanatakiwa kuzirudisha
kwa wakati .
“Yote
haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za
watu nimekuwa nikimpigia simu Diamond hataki kupokea simu zangu, lakini
kama alitaka kunidhulumu ni bora angejiunga mwenyewe na hawa Vicoba ili
apate mkopo na kufanya mambo yake au kama aliona hawezi kwa kujishtukia
basi angetumia ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na hakuna mtu yeyote
angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la watu,” alisema.
Hata
hivyo Diamond ambae kwa sasa yupo nchini Burundi kwa ajili ya ziara
yake kimuziki, tayari ametumiwa taarifa na jeshi la polisi kwa barua ya
wito kufika kituoni pindi atakaporejea nchini, huku mama yake mzazi
akifikishiwa ujumbe huo nyumbani kwake.
Wema
ambae alimwekea dhamana, yupo katika kipindi kigumu ambacho kinaweza
kupelekea kufilisiwa mali zake ambazo aliziandikisha wakati wa kuchukua
mkopo huo ili ziweze kufidia deni hilo.
Kwa
mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo ambae aligoma kutajwa jina lake
gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema alifika katika ofisi zao zilizopo
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili apewe muongozo lakini alipotakiwa
kufuata taratibu za kiofisi kama wanachama wengine wanavyofanya katika
vikundi, hakukubaliana na utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia
tovuti .
MTANZANIA
ilimtafuta Meneja wa Wema, Martin Kadinda, ambae alieleza hajui
chochote kuhusu kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba apewe muda kumtafuta
msanii huyo ili aweze kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, lakini
hakueleza nini kilichojiri na kusisitiza asubiriwe.
Gazeti
hili halikuishia hapo, lilimsaka Meneja wa Diamond, Babu Tale, ambae
alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote
No comments:
Post a Comment
paulmkale