Showing posts with label WEMA SEPETU. Show all posts
Showing posts with label WEMA SEPETU. Show all posts

Wema sepetu Atimuliwa kenye nyumba kisa Skendo ya maji na Umeme!

UFALME umeanguka! Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe ‘nyuzi’ hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa shilingi milioni 280, fuatana na Ijumaa Wikienda. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Wema amekumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa Desemba 18, mwaka huu. 
 
SIKIA CHANZO
 “Jamani mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi limemtokea puani, maana kwenye umeme pekee yake nasikia anadaiwa zaidi ya shilingi milioni nane (8,000,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa.”
 BABA MWENYE NYUMBA
AINGIA KATI “Sasa baba mwenye nyumba ameingilia kati. Ameamua kulipa yeye deni hilo lakini akamtaka Wema ahame haraka  kwenye nyumba yake,” kilisema chanzo.

 SIKU YA TUKIO Paparazi wetu alizidi kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa, muda huo tayari kuna lori aina ya Toyota Canter linahamisha vitu nyumbani kwa Wema na kwamba, kuna kila dalili anahama baada
ya baba mwenye nyumba wake kumtimua.




 PAPARAZI NYUMBANI KWA WEMA
Ilibidi paparazi wetu akimbie kwa pikipiki iendayo kasi mpaka nyumbani hapo na kukuta kweli lori likibeba vitu mbalimbali huku wabebaji wakitokwa jasho chapachapa. Gari hilo lilisimama kwenye lango kuu la kuingilia ndani ya nyumba hiyo huku likiwa na shehena ya mafurushi ya mizigo. Wakati paparazi wetu akiwa kwenye hali ya mshangao, aliendelea kuona mizigo mbalimbali ikitoka ndani ya mjengo huo huku vyombo anuai vya ndani, kama kabati na baadhi ya makochi yakiwa nje ya nyumba hiyo yakisubiri kupakiwa tayari kwa  safari ya kumuondoa Wema kwenye mjengo huo. 


WEMA HAYUPO 
Swali la kwanza kwa wabebaji hao kutoka kwa paparazi wetu ni wapi alipo Wema. “Unamtaka Wema wa nini wakati
unajua hayupo hapa, kwanza wewe nani?” alikuja juu mpakiaji mmoja.

PAPARAZI ANUSURIKA KIPIGO
Katika hatua nyingine isiyokuwa ya kawaida, wapakiaji wengine walitaka kumshushia kipigo paparazi wetu baada ya kuona mwanga wa kamera wakati akichukua picha kadhaa kwa ajili ya ushahidi. WALIKOHAMIA Uchunguzi wa awali, Wema amehamia Mbezi Beach, Dar. Hata hivyo, tangu sakata la wizi wa maji na umeme, Wema hajawahi kulala na kuamka ndani ya nyumba  hiyo huku habari zikisema amekuwa akiishi mahotelini kama ‘digidigi’. 


KWA NINI WEMA ALISEMA NYUMBA  NI YAKE? “Kuna watu wengi walikuwa hawatambui kwa nini Wema awali alisema hii nyumba ni yake. Mwanzo wakati anahamia, pia alikuwa ana mazungumzo na baba mwenye nyumba kwamba ainunue lakini watoto wakagoma hivyo Wema akawa analipa kodi kila mwaka.

WEMA, PETIT MAN Juzi, Wema hakupatikana hewani ili kujibu madai hayo, lakini mmoja wa watu wake wa karibu, Petit Man alikumbana na paparazi wetu katika klabu moja jijini Dar, alipoulizwa kuhusu mambo hayo alikiri Wema kuhama kwenye nyumba hiyo. “Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beachn alisema Petit.

Huu Ndio Waraka Mzito Wa Siri Aliouandika Wema Sepetu Kuhusu Maisha Yake na Tatizo Linalomsumbua>

Wema Sepetu ni mwigizaji staa wa Tanzania hakuna asiejua, Wema Sepetu ni Miss Tanzania 2006 na ni miongoni mwa mastaa wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, hakuna asiejua…… ila tatizo linalomsumbua kwa sasa inawezekana kuna wengi wasiolijua.
Amekua akisumbuliwa na tatizo la kutoweza kushika ujauzito ambapo baada ya ukimya mwingi, Wema ameamua kuongea yafuatayo kwa wote wanaombeza kutokana na tatizo lenyewe.
Amesema >>> ‘Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana… But sina… Na siwezi kumkufuru mwenyezi mungu…. Au mngependa niwe nawaambia jinsi ninavyo hangaika usiku na mchana kupata mtoto wangu mwenyewe… Is dat wat u want…? kila ntakachofanya kwa ajili ya tumbo langu basi nitangaze… Au mnadhani siumii mnavyosema kuhusu maswala ya mtoto‘

Sentensi ya pili >>> ‘Kumbukeni na mimi pia ni binaadam… nina moyo kama nyie… au mnadhani napenda kuona wenzangu wana watoto au wana ujauzito alafu mimi sina hata wa kusingiziwa… mnaona nafurahia sio…. hivi mna nini jamani… yaani mtu unaweza weka post kwa nia nzuri then people jus come from nowea wanaanza kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza umemkosea nini mwenyezi Mungu‘
‘Kwani kuna niliemkosea yoyote mpaka muanze tu kunikashif na kunitolea maneno mazito namna hio… Kisa mtoto… mnadhani naipenda hii hali… hata mimi natamani kuitwa mama na hakuna kinachoniuma kama hicho…. So mnadhani sijui kama umri unaenda na maisha yenyewe sikuhizi mafupi anytime we die… Mnafikiria nisingependa kuacha hata ka copy kangu siku ndo Mungu anasema ananichukua’
‘Hata mimi natamani ningekuwa napiga picha niko na mwanangu… I want dat with all my life but I cant…. Sitokaa nimkufuru Mungu wangu hata siku moja maana sijui ni kitu gani kaniandikia… But just dont rub it in… It hurts… And im jus a human being like each and everyone of u….

Video : Wema Sepetu - In My Shoes S02EP11

Tizama hapa kipindi cha WEMA SEPETU (@wema_sepetu) ”IN MY SHOES” S02EP11HOST & EXECUTIVE PRODUCER Wema Sepetu
PRODUCER Endless Fame Production
CAMERA & EDITOR Eric Ndeki
CREATIVITY MANAGER Martin Kadinda
SOCIAL NETWORK CO-ORDINATOR Best Werema "Bestizzo"

Haya ndo majibu ya Ommy Dimpoz Kuhusu picha alizopiga na Wema X wa D

Msanii wa bongo fleva, Ommy Dimpoz, amefunguka kuhusiana na picha zilizozua utata na kuzozagaa mitandao zikimuonesha akiwa kitandani na msanii wa filamu Wema sepetu.

Ommy amesema kuwa hana maelezo zaidi ya kuzungumza zaidi ya kusema kuwa hajui ni muda upi zilipigwa picha hizo.

Wiki hii picha hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua maswali kuwa Ommy Dimpoz, ameamua kujiweka kwa Wema, baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platinum."Ni picha tu mimi naona kama ni picha zingine tu za kawaida, sasa nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana stori kwasababu mimi naona sio mara yangu kwanza kupiga picha na Wema hata uki google utaona tunapicha nyingi sana kwa hiyo sijaelewa kwanini zimeleta stori

May be nafikikiri zilizotengeneza stori zaidi ni hizi ambazo zinaonesha tuko chumbani kwasababu mimi nilikuwa nimelala kiukweli na tulikuwa tunakaa kwenye apartment moja nilikua nimeshtukia picha zipo kwenye mitandao unajua unavyokaa kwenye apartment kwasababu tulienda kwenye matembezi binafsi na washikaji wengine tulikua wengi wengi kidogo tulienda South Africa unajua mnavyokaa kama familia kunakuwa na mambo ya utani utani nimeshtukia tu picha zimeenea kwahiyo hata watu wakiniuliza ninawambia wamuuliza aliyepiga picha hizo," Alisema Dimpoz.

Wengi wanafahamu kuwa wewe ni mshikaji wa Diamond Platnumz imekuaje sasa hivi kuonekana kwenye picha na Ex wa Diamond Platnumz,Wema Sepetu…?”

Ommy Dimpoz ; “…Sidhani kama kuna tatizo kwasababu hawa wote ni watu wangu nimefahamia nao siku nyingi nimekuwa nao karibu katika kipindi tofauti kabla hawajakuwa kwenye uhusiano mimi tayari ni watu wangu sidhani mimi nianze kuelezea sijui ooh nilikuwa labda na Wema sehemu, Wema ni mshikaji wangu tangia siku nyingi kwa hiyo hata kama alikuwa katika uhusiano na Diamond yakatokea mahusiano yao pengine hayapo sasa hivi hayawezi kunifanya mimi kuharibu ushikaji wangu kwasababu hivyo ni vitu vyao personal…"Alisema.


Wema Sepetu (@wema_sepetu) ”IN MY SHOES” S02EP10(VIDEO)

Mwigizaji staa wa Tanzania, Wema Sepetu hukutana na watu wake wa nguvu kila wiki kupitia show yake ya TV (Eatv) inayohusu maisha yake pamoja ishu nyingine zinazomuhusu time hii amekuletea in my shoes ya msimu wa pili iliyopo katika nafasi ya kumi.

Itazame #In my Shoes msimu wa pili episode 10 kwa ku play hapa

Haya hapa maneno ya Wema Sepetu kuhusu inshu ya kumfungulia kesi Diamond.

Zilianza kwa kusikika taarifa kwa chinichini ila leo taarifa ikatoka mara baada ya kusambaa zaidi kwa watu na mitandao ya kijamii habari kuwahusu wawili hawa wanao sikika nchini.

MKALI wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu ‘Wema’, amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, kwa kumtapeli kiasi cha Sh milioni 10

 Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili, Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay akidai kuwa alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa makubaliano ya kazi na kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume makubaliano yao. Muhusika mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu wanamtupia lawama kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai kuwa amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia dhamana na taasisi Focus Vicoba kuchukua fedha hizo. “Naona watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi Diamond, pasipo kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali ni mkopo ambao niliingia dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo ya Vicoba. “Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema. Mrembo huyo alieleza muda waliiopeana ahadi ya kurudisha fedha hizo umepita na Diamond haoneshi dalili ya kuzirejesha wakati wanatakiwa kuzirudisha kwa wakati . “Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu Diamond hataki kupokea simu zangu, lakini kama alitaka kunidhulumu ni bora angejiunga mwenyewe na hawa Vicoba ili apate mkopo na kufanya mambo yake au kama aliona hawezi kwa kujishtukia basi angetumia ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na hakuna mtu yeyote angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la watu,” alisema. Hata hivyo Diamond ambae kwa sasa yupo nchini Burundi kwa ajili ya ziara yake kimuziki, tayari ametumiwa taarifa na jeshi la polisi kwa barua ya wito kufika kituoni pindi atakaporejea nchini, huku mama yake mzazi akifikishiwa ujumbe huo nyumbani kwake. Wema ambae alimwekea dhamana, yupo katika kipindi kigumu ambacho kinaweza kupelekea kufilisiwa mali zake ambazo aliziandikisha wakati wa kuchukua mkopo huo ili ziweze kufidia deni hilo. Kwa mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo ambae aligoma kutajwa jina lake gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema alifika katika ofisi zao zilizopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili apewe muongozo lakini alipotakiwa kufuata taratibu za kiofisi kama wanachama wengine wanavyofanya katika vikundi, hakukubaliana na utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia tovuti . MTANZANIA ilimtafuta Meneja wa Wema, Martin Kadinda, ambae alieleza hajui chochote kuhusu kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba apewe muda kumtafuta msanii huyo ili aweze kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, lakini hakueleza nini kilichojiri na kusisitiza asubiriwe. Gazeti hili halikuishia hapo, lilimsaka Meneja wa Diamond, Babu Tale, ambae alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote

WEMA AUZA GARI LA DIAMOND, ADAI HATAKI KUANZA MWAKA NA GUNDU... NI LILE ALILOZAWADIWA KWENYE BETHIDEI YAKE

‘Diamond Platnumz’ akiwa na aliyekuwa mwandani wake Wema Isaac Sepetu ‘Madam’. Lile gari jipya aina ya Nissan Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limezua mapya ambapo baada ya kudai linamchefua sasa anadaiwa kuwa analiuza kwa kigezo kwamba hataki gundu mwaka huu mpya wa 2015.
Gari jipya aina ya Nissan Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ KUMBE LIPO KWA DALALI Habari za kiwango kutoka kwa mnyetishaji wetu zilidai kwamba gari hilo lipo kwa dalali wa kike maarufu ajulikanaye kwa jina moja la Tindwa kwa ajili ya kulitafutia mteja. NI KISASI? Ilidaiwa kwamba, Wema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa ana kisasi na hasira kwa Diamond kwa kuwa jamaa huyo kwa sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Uganda, Zarinah Hassani ‘Zari au The Boss Lady’. “Watu wanadhani Wema anafurahishwa na Diamond kutupia mapicha na Zari baada ya kuwasifia juzikati. “Ukweli ni kwamba hivi sasa Wema anakereka sana na jinsi Diamond anavyoweka mapicha yake na Zari wakiwa sehemu mbalimbali na anaona kuwa na gari ambalo amepewa zawadi na Diamond ni kujipa kero zisizokuwa na sababu hivyo ameamua kuliuza,” kilisema chanzo hicho.Aliyekuwa mwandani wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Wema Isaac Sepetu ‘Madam’. HALIJAPATA MTEJA Mpashaji wetu huyo alizidi kunyetisha kwamba pamoja na gari hilo kuwa sasa bado liko sokoni lakini halijapatia mteja wa kulinunua kitu ambacho kinazidi kumkera Madam. “Bado gari halijapata mteja ‘so’ kitendo hicho kinamkera sana Wema kutokana na gari hilo kutouzika mapema kwa maana kila anapoliona hajisikii vizuri kabisa,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazeti kwani ni ‘besti’ mkubwa wa Wema.
WEMA ANASEMAJE? Baada ya kupewa ubuyu huo, gazeti hili lilimsaka Wema ambaye alipopatikana alidai yupo bize akiandaa shoo zake za mkoani Dodoma na Morogoro. “Ngojeni kwanza nimalize shoo zangu za mikoani. Kwa sasa nipo Dodoma nikimaliza naenda Morogoro,” alisema Wema kwa ahadi kuwa atafafanua suala hilo vizuri akitulia. TUMEFIKAJE HAPA Diamond alimzawadia Wema gari hilo lenye thamani ya Sh. milioni 36, siku ya bethidei ya mwanadada huyo iliyofanyika Septemba 28, mwaka jana. Siku chache baadaye Wema alidai kummwaga jamaa huyo huku akieleza kwamba hapendi kuliona wala kulitumia gari hilo kwani lilikuwa likimzidishia chuki juu ya jamaa huyo.

Wema Sepetu (@wema_sepetu) “IN MY SHOES” S02EP06 My Birthday

Ulipitwa na show ya Wema Sepetu (@wema_sepetu) “IN MY SHOES” S02EP06 My Birthday..? Ingia hapa kutizama

WEMA SEPETU- “IN MY SHOES” S02EP05(VIDEO)

Je ulimiss show ya WEMA SEPETU (@wema_sepetu) “IN MY SHOES” S02EP05..? hebu ingia hapa>>