MJINI bwana! Habari nyingi huanzia kwenye mikeka, siku hizi wenyewe
wamezimebatiza jina la ‘Ubuyu’ ambapo kwa sasa ishu kubwa inayozagaa
mitaani ni mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ kupachikwa mimba na mbunge
maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Bunge la 11 (jina kapuni kwa
sasa), vyanzo vinasema.
Pitapita ya sikio la Gazeti la Ijumaa
katika Jiji la Dar es Salaam, hivi karibuni ilikutana na Ubuyu huo kuwa
mwigizaji huyo amenasa ujauzito wa mwanasiasa huyo ambaye ni kijana
mwenye utajiri mkubwa anayetajwa kwa sasa kumiliki vilivyo penzi la
Madam.

KUMBUKUMBU KABLA YA HABARI
Kwa
muda mrefu, Wema amekuwa akihaha kusaka mtoto baada ya kupitia kwenye
uhusiano na wanaume tofauti akiwemo Yusuph Jumbe, Steven Kanumba
(marehemu), Nasibu Abdul ‘Diamond’ na CK (yule kigogo).
Akiwa
kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume hao kwa hesabu yake na nyakati
tofauti, mara kadhaa msanii huyo maarufu amekuwa akikebehemiwa na
mahasimu wake kuwa ni mgumba jambo ambalo limekuwa likimhuzunisha.
HABARI KAMILI
Ijumaa
baada ya kuzinasa habari za ujauzito wa msanii huyo, lilijongea kwenye
vyanzo vyake na kukutana na ushuhuda huu kutoka kwa rafiki wa karibu wa
Wema ukisema: “Suala la mimba sijui lakini Wema na mheshimiwa wana
uhusiano.
“Ukaribu wao ulianza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu (Wema alikuwa
akimnadi mgombea urais wa CCM, John Magufuli), mpaka leo wanaendelea.”
MIMBA KABAAH!
Baada
ya chanzo cha karibu na Wema kutoboa mfereji wa uhusiano na kuliacha
suala la ujauzito kwenye sintofahamu, wachapakazi wa Ijumaa waligeuza
masikio yao upande wa mheshimiwa mbunge ili kupata ubuyu mwingine ambapo
suala la mimba lilitajwa waziwazi.
“Sitaki kunukuliwa ila mimi
nimemsikia mheshimiwa akidokeza kuwa Wema ni mjamzito, kwangu mimi kama
rafiki yake naona ni jambo jema, hiyo ndiyo kazi ya mwanaume
kaka...hahahahaha!” Mmoja kati ya marafiki wa mbunge huyo alisema na
kumalizia kwa kicheko.
WEMA NA MBUNGE FULL KICHEKO
Inaelezwa
na vyanzo vyetu kuwa baada Wema na mbunge huyo kuwa wazazi watarajiwa
wote kwa pamoja wamekuwa na furaha ya aina yake huku kila mmoja
akimsisitiza mwenzake kuwa makini ili upepo mbaya usipite kati yao.
Aidha,
katika hali inayoashiria kuwepo kwa kitu cha tofauti kwa msanii huyo
aliyepata kuwa Miss Tanzania 2006, hivi karibuni aliandika kwenye
akaunti ya Instagram kuwa anayo sapraizi ya nguvu kwa mashabiki wake.
Baadhi
ya wadau wa masuala ya burudani wamehusisha sapraizi aliyoitangaza Wema
na habari za ujauzito wake unaotarajiwa kumaliza kejeli juu yake kuwa
yeye ni sawa na mti usiozaa kwamba hauna thamani.
MBUNGE NI TAJIRI MKUBWA
Mbali
na umaarufu wa mbunge huyo timu ya Ijumaa ilijiridhisha kuwa mwanasiasa
huyo ni tajiri anayemiliki migodi ya madini na kufanya biashara
mbalimbali zikiwemo za usafirishaji mizigo na abiria anazofanya kupitia
magari yake.
Kutokana na utajiri huo, habari zinadai kuwa mbunge
huyo ndiye anayempa jeuri ya fedha Wema ambayo inamfanya aishi maisha ya
‘nyodo’ kama wasemavyo watoto wa mjini.
WEMA, MBUNGE WATAFUTWA
Katika
kukamilisha weledi wa habari, gazeti hili lilimtafuta mbunge huyo kwa
njia ya simu ili azungumzie ishu hiyo lakini hakuweza kupatikana hewani
jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa jina lake kuhifadhiwa.
Kwa
upande wa Wema naye hakuweza kupatikana kwa namba zake za simu sambamba
na ile ambayo chanzo chetu kilisema ni mpya jambo linaloifanya habari
hii kuwa na mwendelezo baada ya kujiridhisha kwa kupata kauli za pande
zote mbili.
AUNT ANENA
Kama haitoshi gazeti hili lilimtafuta
shosti wake wa karibu na Wema, Aunt Ezekiel ili naye afunguke kidogo juu
ya madai ya ujazito wa rafiki yake ambapo mahojiano yalikuwa hivi:
Ijumaa: Mambo anti’ake?
Aunt: Safi cha umbea wangu, nipe mpya.
Ijumaa: Naona shosti yako Wema karudi ili umpe mafunzo ya kulea mimba, mpe hongera zake, kushika mimba ya mbunge si jambo dogo.
Aunt: Kwani kakuambia yeye mwenyewe? Kwanza niko naye hapa, anasema simu zako amekuwa anaziona lakini hataki kupokea.
Baada ya mazungumzo hayo ilisikika sauti ya Wema ikisema: “Tena mwambie ni ya miezi 6, tatizo nini?”
CHANZO: GAZETI LA IJUMAA