Diamond Platinumz akacha shoo ya zari.


Habari ya mjini! Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amezua utata kwa mashabiki wake baada ya kukacha kuzama kwenye pati iliyokuwa imeandaliwa na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Guvnor jijini Kampala, Uganda ambapo wawili hao walikwenda pamoja kwa lengo la kushirikiana kwenye makamuzi ya shoo ya pati hiyo iliyokwenda kwa jina la Zari All White Ciroc Party.
 Zari All White Ciroc Party
Ilielezwa kwamba, tofauti na matarajio ya wengi, Diamond hakuonekana ukumbini badala yake aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga akawa anajitanua ukumbini humo akiwa na rafiki zake huku Pedeshee Jack Pemba wa Bongo akigandana na Zari muda mwingi.
Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’, Ijumaa Wikienda kama kawaida yake lilimtafuta Diamond kwa lengo la kutaka kujua kilichomkwamisha kwenda kwenye makamuzi ya mzazi mwenzake huyo ambapo alisema alishindwa kuhudhuria baada ya promota wake kumzuia kwenda ‘kumkampani’ Zari akihofia kuzorotesha makamuzi yake yaliyopangwa kufanyika siku iliyofuata kwenye Viwanja vya Lugogo Cricket Oval jijini Kampala.
 ZARI834
“Nilikuwa na hamu mno ya kumpa kampani mama Tiffah lakini nilizuiwa na promota wangu kuhofia kama ningeonekana ukumbini basi ningeweza kumvurugia shoo yake maana aliniambia nisionekane kabisa, nadhani tageti yake ilikuwa ni kuhakikisha watu wananishuhudia siku ya shoo yangu tu,” alisema Diamond.
Kufuatia kukosekana kwa Diamond kwenye pati hiyo, watu walijikuta wakinong’ona ukumbini wakitaka kumuona kwani walishajua kuwa yupo jijini Kampala.

No comments:

Post a Comment

paulmkale