MUSA MATEJA, Risasi Jumamosi
Dar es Salaam: Hii ni habari ya kipekee (Exclusive Story)! Mastaa
wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana,
Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wanadaiwa
kumwagana, Risasi Jumamosi ndilo gazeti pekee linaloweza kuthubutu
kukupa mchapo kamili.
Habari ya mjini kwa sasa ni juu ya wawili
hao ambao walikuwa gumzo kwa watoto wa mjini, kwa kila mmoja kuchukua
hamsini zake na kufanya yake tofauti na walivyokuwa awali huku chanzo
cha kutengena kwao kikitajwa kuwa ni wazazi wa sehemu zote mbili
kutoridhiana.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao,
mbali na ishu ya wazazi, hivi karibuni Jokate na Kiba waliingia kwenye
gogoro kubwa la kimapenzi baada ya kufumaniana kwenye simu, jambo ambalo
limeendelea kutokea huku jamaa akiongoza kukutwa na meseji kwenye simu
yake za mwanamke mmoja anayedaiwa kuishi nje ya Tanzania.
BOFYA HAPA KUSIKIA CHANZO
“Ukisema nikusimulie juu ya kumwagana kwa Jokate na Kiba basi tunaweza
kukesha ila mbali na mambo ya wazazi, kwa kifupi tu ni kwamba, hawa watu
wameingia kwenye mgogoro na kilichokuwa kikiwagombanisha mara nyingi ni
uhusiano wao wa zamani.”
KIBA ANA DEMU?
“Mara kadhaa Jojo
(Jokate) amekuwa akimlalamikia jamaa (Kiba) kuwa ana demu nje ya nchi
ambaye amekuwa akimtundika katika mitandao ya jamii na kujinadi kuwa
ndiye mkewe tofauti na wengi wanavyojua kuwa Jokate ndiye mtu wake.
“Mbali
na hilo, sasa kuna suala la familia zao kuonesha hali ya kutokubaliana
na wao kuoana hasa upande wa Jokate ambao ulionesha msimamo mkubwa
kutomtaka hata kidogo Kiba, mambo hayo yamekuwa ni chagizo kubwa katika
kuhatarisha mapenzi yao hivyo kufikia hatua hata ya wao kutoendelea
kupendana kwa dhati kama ilivyokuwa mwanzo wa penzi lao.”
VIKAO VYAGONGA MWAMBA
“Tofauti na watu walivyozoea kuwaona pamoja, kwa sasa wametibuana na
hapa tunapozungumza tayari kuna vikao kibao huko nyuma vilishakaa ili
kunusuru penzi lao lakini imeshindikana maana kila mmoja sasa hivi
anajifanyia mambo yake na hakuna dalili za kurudiana.
“Kiba anaonekana ameshajiingiza kwenye penzi la demu wake wa zamani huku Jokate naye akiwa ‘in love’ na mtu wake mwingine.”
MPANGO WA KUZAA WAYEYUKA
“Kitambo tu nimekuwa nikiwaambia kwa staili waliyokuwa nayo hakika
wasingeoana hata kama ukiweka pembeni suala la dini zao kutoendana,
maana kuna siku niliwasikia wakiambiana hata kama wazazi wakigoma wao
wangefanya kila juhudi hata wazae pamoja tu.
“Lakini ukweli ni
kwamba ilishindikana baada ya kuanza kugombana mara kwa mara, pamoja na
kwamba Jokate alikuwa akikubalika kwa asilimia zote kwa mama Kiba na
hata ndugu wengi wa Kiba walionekana kumpenda waziwazi,” kilisema chanzo
hicho.
KIBA AFUNGUKA
Baada ya kupenyezewa mchongo huo, gazeti
hili liliingia mzigoni kumtafuta Kiba ili atoe la moyoni juu ya madai
hayo ya kumwagana na Jokate ambapo alipopatikana alisema kuwa haoni
sababu ya kuzungumzia ishu hiyo kwani ni mambo binafsi.
“Kusema
kweli ishu hii mimi sina uwezo wa kuiongelea zaidi kwa sasa kwani ni
mambo binafsi sana na sioni faida ya kuzungumzia vitu ambavyo havina
maana.
“Kwanza sioni nini cha kuongelea hapa kwani kila jambo lina
mipaka yake,” alisema Kiba akikataa kuulizwa zaidi juu ya suala hilo.
JOKATE VIPI?
Kwa upande wa Jokate alipotafutwa kwa siku kadhaa ili azungumzie sakata
hilo kwa ufasaha hakupokea simu ya mwandishi wetu hadi gazeti linaingia
mitamboni.
PENZI LA JOKATE NA KIBA
Awali zilipovuja habari za
penzi la Jokate na Kiba wote walikanusha, kadiri siku zilivyosonga
ndivyo walivyozidi kuwa gumzo kwa mashabiki wao waliofurahishwa na
‘kapo’ yao huku wakionekana kwenye viwanja mbalimbali vya starehe wakiwa
kimahaba lakini sasa mambo yanaonekana kwenda mrama.
No comments:
Post a Comment
paulmkale