Ili kuhakikisha hasalitiwi katika penzi lake jipya, mkali wa Bongo
Fleva Baraka Da Prince, ameajiri baunsa kwa ajili ya kumlinda mpenzi
wake Salma Jabu ‘Nisha’ popote anapokwenda.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa Baraka amefanya hivyo
kutokana na wivu uliopitiliza. Nisha alikiri kuwekewa baunsa ambaye ni
ndugu wa mpenzi wake, hivyo kila anapokwenda lazima awepo kwa sababu
anahofia kusalitiwa.
“Mpenzi
wangu Baraka ana wivu sana na ameniwekea baunsa ambaye naenda naye kila
sehemu ni mwanaume aliyekamilika, hana upungufu wowote na mimi sijali
kuhusu skendo, haziniumizi kwa sababu tunaaminiana, najua hao ni
marafiki wa kawaida tu,” alisema Nisha anayetesa na Filamu ya Kiboko
Kabisa.
No comments:
Post a Comment
paulmkale