Hii ndiyo style mpya ya Nywele aliyoamua kuja nayo Joti 2015.
Asilimia kubwa ya mastar wengi wa duniani huwa wanapenda kutengeneza
kitu ambacho kitakua tofauti na wengine ili kumtengenezea utambulisho
wake popote anapokuwepo.
Tumeona style kadhaa za mavazi ambayo yanapovaliwa na mastar huwa
yanachukua chart kwa kuvaliwa pia na watu wa kawaida ambao huwa
wanavutiwa nayo.
Kingine ni style ya nywele ambazo mastar wamekuja nazo ikiwemo kiduku
ambapo kwa sasa mastar wengi wananyoa hivyo,kuna wengine wanaachia
nywele zinakua nyingi style hii wengi wao huita ‘Mwembe’ kwa wingi wa
nywele kichwani.
Star kutoka kundi la Original Komed Joti yeye mwaka 2015 kaamua kuja
na style hii ambayo hajasema inaitwaje ambapo kwenye ukurasa wake wa
Instagram alipost picha akiwa ananyoa na alipomaliza.
Katika post yake ya kwanza aliandika>>’Kwaheri 2014′ hii
alionekana akinyoa na katika post nyingine aliandika>>’Now karibu
2015,karibu babaaa…..my new style’.
No comments:
Post a Comment
paulmkale