Manchester City kumsajili Wilfred Bony .

Mabingwa watetezi wa ligi ya England Manchester City wanatarajiwa
kuanza mazungumzo na klabu ya Swansea city wakiwa na lengo la kumsajili
mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfred Bony.
City wamepanga kumsajili mshambuliaji huyo na wanatarajiwa kupeleka ofa ya kwanza ambayo inaaminika kufikia paundi milioni 25 .
City wanakuwa timu ya kwanza kupeleka ofa kwa ajili ya mshambuliaji
huyo huku wakifahamu kuwa anasakwa na timu kadhaa zikiwemo Real Madrid
na Liverpool.
Mwenyekiti wa Swansea Huw Jenkins amekanusha habari za kuwepo kwa
mpango wa kuuzwa kwa mchezaji huyo japo tayari mazungumzo baina ya
viongozi wa Man City na wawakilishi wa Bony yameanza baada ya mkutano
uliofanyika hapo jana (jumatano) na kama kila kitu kikienda kama
ilivyopangwa City itamsajili mchezaji huyo .

Bony akiwa na timu yake ya taifa ya Ivory Coast ambako amerithi nafasi ya mshambuliaji aliyestaafu Didier Drogba.
Hata hivyo endapo usajili huo utakamilika Manchester City haitaweza
kumtumia Bony kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu kutokana na
adhabu ya kukiuka misingi ya sheria za usimamizi wa fedha maarufu kama
Financial Fair Play ambako hawaruhusiwi kuongeza mchezaji mwingine
kwenye kikosi chao cha ligi ya mabingwa .
Bony anatazamwa na City kama mtu atakayekuwa mbadala wa yoyote kati
ya washambuliaji wao watatu Stevan Jovetic, Sergio Aguerro na Edin Dzeko
ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha ambayo
yameikosesha City washambuliaji kiasi cha kulazimika kutumia wachezaji
kama David Silva na James Milner kwenye nafasi ya ushambuliaji .
No comments:
Post a Comment
paulmkale