Mabingwa wa ulaya Real Madrid hii leo (jumapili) wameuanza vibaya
mwaka 2015 baada ya kukubali kipigo cha 2-1 toka kwa Valencia katika
mchezo wao wa 17 wa ligi kuu ya Hispania uliopigwa kwneye uwanja wa
nyumbani wa Valencia Estadio Mestalla.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwa Real Madrid tangu
kuanza kwa mwaka mpya Real walianza kwa kasi wakifunga bao kwenye dakika
ya 14 mfungaji akiwa Cristiano Ronaldo akifunga kwa mkwaju wa penati
baada baada ya mshambuliaji wa Valencia Alvaro Negredo kuushika mpira
kwa mkono .
Cristiano Ronaldo akiifungia Real Madrid bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati .
Bao hilo kwa Real Madrid lilidumu kwa muda mrefu kidogo na Valencia
walisawazisha mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya dakiak 7 kwenye
dakika ya 52 mfungaji akiwa Antonio Baraggan ambaye alipiga shuti kali
lililowazidi mabeki Sergio Ramos na Pepe pamoja na kipa wao Iker
Casillas .
Bao hilo liliamsha mashambulizi ya Valencia na haikuwachukua muda
kabla ya kufunga bao la pili mfungaji akiwa beki raia wa Argentina
Nicolas Otamendi ambaye alifunga kwenye dakika ya 65 ya mchezo akimaliza
kwa kichwa kona iliyopigwa na Dani Parejo .
Wachezaji wa Valencia wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Antonio Baraggan .
Real Madrid walijaribu kusawazisha bao hilo bila mafanikio yoyote na
hadi dakika 90 zinamalizika Valencia waliondoka na pointi zote 3 .
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Real Madrid kupoteza rekodi yake ya
kushinda michezo 22 mfululizo huku wakishindwa kuifikia na kuizidi
rekodi ya timu ya Brazil ya Coritiba ambayo iliwahi kucheza mechi 24 za
kiushindani bila ya kupoteza mechi hata moja .
Wachezaji wa Real Madrid wakiwa wanatoka uwanjani kwa majonzi baada ya kufungwa na Valencia .
No comments:
Post a Comment
paulmkale