Soma hapa kisa cha ugomvi wa Messi na Kocha wake
Habari za kuwepo kwa uhusiano mbaya kati ya nyota wa Barcelona Lionel
Messi na kocha wake Luis Enrique mpaka sasa sio mpya masikioni mwa
mashabiki wa soka barani ulaya baada ya matukio kadhaa ambayo yamekuwa
yakitokea ndani ya klabu hiyo ya Nou Camp.
Tetesi zaidi zinadai kuwa kocha Luis Enrique amepewa mechi mbili
kuokoa kazi yake jambo ambalo Barcelona imekanusha laki ni hakuna
asiyefahamu kuwa Messi na kocha wake hawaelewani .
Chanzo cha ugomvi baina ya wawili hao kimefahamika baada ya ripoti
kadhaa toka kwa wtau walioko karibu na klabu hiyo kufichua kuwa ugomvi
huu ni mkubwa kuliko inavyodhaniwa na umefikia hatua mbaya .
Ripoti tofauti zinasema kuwa Messi na kocha wake waligombana siku ya
ijumaa wiki iliyopita na ugomvi ulikuwa mkubwa kiasi cha wawili hao
kukunjana na kutaka kupigana kabla ya kuachanishwa na wachezaji wa
Barcelona.
Messi ambaye alichelewa kujiunga na kambi ya Barcelona baada ya
kutoka kwenye mapumziko nyumbani kwao Argentina aliingia mazoezini siku
hiyo ya ijumaa na kuungana na wenzie ambao walikuwa wakifanya mazoezi ya
kucheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe huku Enrique akiwa refa .
Katika mazoezi hayo Messi alichezewa rafu ambayo alitaka kupewa
adhabu ndogo lakini Enrique hakupuliza filimbi jambo ambalo lilimkera
Messi na kumfanya aanze kumshutumu Enrique .
Baada ya mazoezi hayo kumalizika Messi alimfuata Enrique na kuanza
kutupiana nae maneno mpaka kufikia kukunjana kabla Neymar hajaingilia
ugomvi huo na kuwatenganisha kabla hawajapigana .
Kufuatia ugomvi huu Enrique alimuacha Messi benchi kwenye mchezo
uliofuata dhidi ya Sociedad na nyota huyo alijibu mapigo kwa
kutohudhuria mazoezi ya jumatatu .
No comments:
Post a Comment
paulmkale