Ommy Dimpoz
mzee wa "Tupogo" , weekend iliyopita alizuiwa uwanja wa ndege wa
Marekani na kurudishwa Tanzania na ndege iliyofata na hivyo
kumsababishia kushindwa kufanya show aliyotegemewa kuifanya siku ya
jumapili ya tarehe 16, Lasvegas.kwa mujibu wa
habari zilizokuwa zimeenea na zilizotoka katoka chanzo cha karibu ,
zilikuwa zinadai kuwa Ommy karudishwa sababu visa aliyokuwa nayo ilikuwa
ni visa isimruhusu kufanya show Marekani bali ilikuwa ni visa ya
kwenda kutembea. Leo hii tumeongea na Ommy ambae amerejea siku ya Jana
"kilichotokea
ni kwamba mimi nilitoka hapa nikaenda mpaka Amsterdam na Amsterdam
nilikuwa na connect flight kutoka Amsterdam kwenda detroit na detroit
kwenda Vegas kwahiyo kufika Amsterdam nilimiss flight ya connect
Amsterdam kwenda detroit kwa hiyo ikabidi ni rebook booking yangu ili
nipate flight nyingine ya kwenda Las Vegas kwa hiyo nikakosa connection
ya kwenda detroit nikapata connection nyingine ya kupitia Minnesota
nilivyofika kule wakati nimefika airport ndege ambayo nilipata
connection na hii ya pili ikawa tayari ilikuwa imenichelewesha kwasababu
ilikuwa inatakiwa inifikishe siku ya show sasa pale kukawa na tatizo
kule watu wa venue siku ambayo waliokuwa wameongea nao" amesema Ommy
Dimpoz
"kwa
hiyo ikabidi waongee kuwa msanii amechelewa lakini tunaomba event
tufanye siku nyingine lakini wale jamaa wakakataa wakasema haiwezekani
na lengo ilikuwa mimi ni perform kwenye hiyo weekend ya rugby kwa
hiyo kutokana na mazingira hayo ikabidi wale watu wa immigration unajua
siku zote ukifika ile ni nchi unavyoingia siku zote lazima kuna maswali
ya security pale lazima uulizwe, unajua watu hawajui kitu kimoja kwamba
kupata visa sio ndio kuingia kwenye nchi ya mtu kwamba ukifika nchi
yoyote hata sisi tunaenda South Africa naona ni nchi ambayo tunaingia
bila visa ukifika airport lazima uulizwe unakuja kufanya nini, unakaa
siku ngapi, kwa hiyo nchi zote utaratibu ndio huo kwa hiyo katika pale
kuulizwa nikawambia naenda Las Vegas kwenye show,kwahiyo wakapiga simu
kule kwa watu wa event pamoja na sehemu ya Venue kwa hiyo watu wa
Venue wakaambiwa kulitakiwa kuwe na show ila msanii hakufika kwa hiyo
wakabidi waongee na promote akasema tumeisongeza kwasababu msanii
amechelewa amemiss flight sasa wakarudi kwangu wakaniambia lengo
lilikuwa uje kwenye hii show na show tayari umeshaimiss kwasababu ya
matatizo ambayo sisi hatutakiwa kuyajua yamesababishwa na nini wakasema
kwamba lakini hapa inaonesha una show nyingine New york tarehe 21
nikawaambia ndio nilikuwa ninayo ila nilipanga nikitoka Las Vegas
naelekea huko" aliendelea kusema
"Wakaniambia
sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusisha
chama cha kisiasa na kama uliona hata kwenye promotion yangu nilikuwa
nimeandika kuwa nitakuwa na show ya miaka 38 ya CCM Marekani, unajua
vyama cha siasa hivi Chadema, CCM wanamatawi yao kule Marekani watu
wanaoishi nje mara nyingi uwa wanafanya sherehe sherehe za Annivesary ,
kwa hiyo wakaniambia kuwa hii visa yako haikuruhusu wewe kuperform kuna
aina ya Visa ya inayoruhusu msanii ku perform kwasababu show yako ni
kama ya kisiasa, kwa hiyo kwa kuangalia hivyo wakaniambia option iliyopo
itabidi nirudi nyumbani kwasababu shughuli iliyokuleta imeshindikana
kwa hiyo unaweza ukaja mwenyewe baadae kwa matembezi yako au kwa nini
lakini hata ikitokea mfano leo nikakatiwa ticket au nikate ticket nirudi
Marekani visa yangu sasa hivi hainiruhusu kwa hiyo ina maana ninataka
kuchukue visa nyingine yenye kibali maalumu chenye kuperform mimi kwenye
show."
No comments:
Post a Comment
paulmkale