Collabo ya K-Cee na Diamond Platnumz"LOVE BOAT" kutoka jumanne ya wiki ijayo.

Jina la Diamond Platnumz lina  uhakika wa kuendelea kutajwa na sauti yake kuendelea kusikika kupitia vituo mbalimbali vya Nigeria na Afrika kwa ujumla kwa kipindi hiki, kutokana na nyimbo alizoshirikishwa na wasanii wa huko kuzidi kuachiwa.

Msanii mwingine wa Nigeria, Kcee ametangaza ujio wa wimbo wake mpya aliomshirikisha Diamond ambao waliurekodi mwaka jana. Wimbo huo uitwao ‘Love Boat’ utatoka Jumanne ijayo 16/06/2015.
Hit maker huyo wa ‘Limpopo’ ambaye pia alishirikishwa na Shetta kwenye ‘Shikorobo’, ameiita collabo hiyo kuwa ni ‘Africa’s Hottest Collabo’.
Kupitia Instagram yake Kcee ameshare cover na kuandika:
“Anticipate Africa’s Hottest collabo out on the 16/06/2015 God bless Africa God bless you all. @diamondplatnumz”
Collabo ambazo zimeshatoka kwa mwaka huu kati ya Diamond na mastaa wa Nigeria ni ‘Nana’ aliyomshirikisha Flavour, pamoja na ile ya Iyanya aliyomshirikisha Diamond ‘I Love You/Nakupenda’.

No comments:

Post a Comment

paulmkale