WAZIRI wa
Uchukuzi, Samuel Sitta ametangaza rasmi nia ya kugombea urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM na kusema ana ari, uwezo na
utayari wa kuiimarisha nchi na kwamba kipindi kimoja tu cha miaka mitano
kinamtosha.
Mbali na
hilo, Sitta amesema akifanikiwa kupata nafasi ya kuongoza nchi
atahakikisha anatenganisha masuala ya siasa na biashara, kwa sababu
ndiyo chanzo cha rushwa kubwa na kufikiwa kwa mikataba mibovu.
Alitangaza
nia yake hiyo jana kwenye eneo la Itetemia (Ikulu) mkoani Tabora ambako
kulikuwa na makao makuu ya mashujaa wa Unyanyembe wakiwemo Isike na
Kiyungi walioendesha harakati dhidi ya dhuluma na unyanyasaji wa
wakoloni.
Pia, neno
‘Ikulu’ asili yake ni Itetemia baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere ilipofika mwaka 1961 kuamua kulitumia neno hilo la Kinyamwezi
liwe mbadala wa maneno ya kikoloni ya ‘State House’ kwa ofisi na makazi
ya mkuu wa nchi ambayo kwa sasa yapo eneo la Magogoni, Dar es Salaam.
“Uimara
wangu kiuongozi nitajumuisha nguvu na maarifa ya wananchi ili tuvuke
salama na pia tutekeleze kazi za maendeleo kwa ufanisi na tija zaidi.
...nakuja kwenu Watanzania kuomba niwatumikie katika nafasi hii ya juu
ya uongozi. Ninayo ari, ninao uwezo na utayari wa kuiimarisha nchi yetu
katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya utawala,” alisema Sitta.
Katika
hotuba yake hiyo, Sitta aliainisha baadhi ya vipaumbele na kuwa
kimojawapo ni kupambana kwa nguvu zote na vitendo vya rushwa kiasi
kwamba akifanikiwa kuingia madarakani atatenganisha masuala ya siasa na
biashara.
Akifafanua
kuhusu hilo, Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania alisema rushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya kwa
uchumi wa nchi yetu ambapo mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi
hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na
hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya fedha
kwa taifa.
“Uchumi
unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayo sasa imeenea mijini na
hata vijijini...kwa hatua ya kwanza hatuna budi kutenganisha biashara
na uongozi.
Mtu
achague kimoja; biashara au uongozi wa siasa. Ikiwa mfanyabiashara
atataka kuingia katika uongozi wa siasa itabidi akabidhi mali na
biashara zake kwa mdhamini atakayeendesha biashara hizo wakati mhusika
anatumikia Umma,” alisema Sitta.
Aliongeza
kuwa kwa sasa baadhi ya wanasiasa na watumishi waandamizi serikalini
wanatumia nafasi zao kujitajirisha kupitia kujipendelea na kuwa jambo
hilo lina athari zake ikiwemo; kuchochea rushwa na usumbufu kwa
wananchi; kupunguza ari ya wafanyabiashara wa dhati na kudumaza
uwekezaji.
Sitta
alitaja hatua nyingine katika kukabiliana na rushwa kuwa ni kutunga
sheria mpya zilizo kali na ambazo zitakuwa na matokeo ya kumzuia mtu
asitamani kusaka rushwa, mali za viongozi zitamkwe kwa uwazi, mali
isiyolingana na kipato na kukosa maelezo ya kutosheleza itaifishwe, kesi
za rushwa ziwe na utaratibu wenye uwazi na tume inayoshughulikia
maadili ya viongozi ipewe nguvu kubwa za uchunguzi na ufuatiliaji wa
mali za viongozi bila kuzuiwa na mamlaka yeyote.
“Sambamba
na kupiga vita rushwa, hatuna budi kuchukua hatua kali dhidi ya hujuma
za uporaji wa maliasili za nchi na rasilimali zake.
Madini,
misitu, vyanzo vya maji, bahari, maziwa namito ni rasilimali ambazo
zisipotunzwa zitatishia uendelevu wa uchumi kwa vizazi vijavyo, kwa
hivyo uhalifu dhidi ya maliasili na rasilimali za nchi itabidi uwekewe
sheria na taratibu kali,” alionya Sitta.
Akieleza
kuhusu vipaumbele vyake vingine, Sitta alisema kwa maoni yake kipindi
cha miaka mitano ijayo kina mwelekeo wa mifarakano katika masuala ya
Muungano, kutetereka kwa mshikamano kunakotokana na chokochoko za siasa
za ushindani, udini na kupanuka kwa tofauti ya kipato na ongezeko la
kundi kubwa hususani la vijana mijini lisilo na uhakika wa ajira.
Kutokana
na hali hiyo, alisema atatumia mchanganyiko wa uzoefu wa uongozi
kutanzua changamoto hizo ikiwemo ya Muungano. Kuhusu hilo la Muungano
alisema kwa sasa zinajitokeza kauli na vitendo ambavyo vinaashiria
kutaka nchi mbili zilizoungana zitengane.
“Kutoka
Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi
ikirejea kuwa na uhuru kamili bila kuwa ni sehemu ya Muungano.
Baadhi ya
wabara nao wanawatazama ndugu zao wa Zanzibar kuwa ni wakorofi
wasioridhika na chochote kitakachofanywa na Muungano na wanahisi kuwa
mfumo wa Muungano uliopo unaipendelea Zanzibar ili hali baadhi ya
Wazanzibari nao wanadai kuwa Bara inapendelewa.”
Sitta
alijinadi kuwa kiongozi anayeweza kuzileta pamoja kambi hizi na kuuokoa
Muungano hana budi kuwa na ufahamu mzuri wa kutosha wa asili, misingi na
manufaa ya Muungano.
“Ushiriki wangu katika serikali yetu tangu awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi yetu unaniweka katika nafasi nzuri ya
No comments:
Post a Comment
paulmkale