BASATA imemfungia Shilole mwaka mmoja, hakuna kufanya muziki
Breaking news zilizoifikia
saa nne usiku wa July 30 2015 kutoka Baraza la sanaa Tanzania (BASATA)
ni kwamba baraza hili limemfungia Shilole kutojihusisha na kazi yoyote
ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika
onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya
wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya
kitanzania kimaadili‘‘BASATA ilipata habari zako,
kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha
tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA
ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu
kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako‘ – BASATA‘Baraza limejiridhisha kwamba
ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji
makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri
ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya
Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa
nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo
kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
paulmkale