Akizungumza katika kipindi cha XXL japo Diamond alionyesha kutotaka kulizungumzia hili alisema:
"Sijawahi kuwa na beef nae hata siku moja na tuko poa"
Kuhusu kuwepo kwa hizi team diamond na Team Kiba, diamond amesema:
"wakati
mwingine ni vitu vinakuwa vinatokea katika kazi ambayo kwa mtazamo
wangu mimi sioni ubaya wowote, unajua kila mtu ana maamuzi ya
kumshabikia mtu anayemtaka yeye, huwezi kumforce mtu awe yanga unakuwa
unamlazimisha, ni vitu kama hivyo, so sidhani kama kuna ubaya wowote,
kwa baadhi ya watu wakiamua kuutumia kiubaya ndo watakuwa wanakosea, kwa
mtazamo wangu naamini panapokuwa na changamoto ndo panafanya muziki
wetu ukue, unakuwa mkubwa lakini sasa ifikie time kama mashabiki, mimi
kwa akili yangu ndogo ninavyohisi wachukue msanii flani wawashindanishe
na wasanii wa nje, kwa sababu ukishindanisha wasanii wa Tanzania kwa
Tanzania haiwezi kuleta impact yoyote katika industry yetu, mimi
nikabidhi davido, flani mkabidhi wizkid, kila mtu akapige ushindi halafu
alete nyumbani."
No comments:
Post a Comment
paulmkale