Bongo Kumekucha! Vanessa Mdee nae atajwa kwenye Tuzo hizi kubwa za Canada.

Sasa Muziki wa Bongo unaenda kuwa On Top, Diamond Platnumz na Vanessa Mdee wanafanya vizuri sana kimataifa kwa sasa! Leo Diamond Platnumz katajwa katika tuzo za International Reggae and World Music Awards (IRAWMA) 2015, na leo tena Vanessa Mdee nae katajwa katika tuzo za African Entertainment Awards (AEA) katika kipengele cha Best International African Female Artist.Katika Mtandao wa Instagram Vanessa Mdee ameandika “Namshukuru Mungu kwa nomination nyingine hii ya #AEA ya Canada. Ni Baraka kusema la ukweli Asanteni guys najua nguvu zenu pia zimechangia haya basi tupige kura. Link iko kwenye bio yangu Twitter @VanessaMdee #AwardSeason”.

No comments:

Post a Comment

paulmkale