Yanga imeizidi kete Simba katika utitiri wa mastraika 8...


YANGA imeizidi kete Simba katika utitiri wa washambuliaji baada ya usajili wa nyota wawili kwa mpigo; Paul Nonga na Issofou Boubacar ‘Garba’ ambao umeifanya kuwa na jumla ya washambuliaji nane, mmoja zaidi ya watani wao.
 

Wakati wadau wa soka wakijadili umuhimu wa Nonga katika jeshi lililosheheni washambuliaji wakali, Yanga wamekuja juu na kusema kuwa na ingewezekana wangeendelea kuongeza wengine kwani wanataka kuwa na kikosi kipana zaidi.
 

Safu ya mbele inaundwa na; Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Garba, Nonga, Matheo Simon na Malim Busungu, wakati huohuo kuna viungo washambuliaji Geoffrey Mwashuiya na  Simon Msuva ambao pia wanao uwezo wa kufunga.
 

Akifafanua kiufundi zaidi, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, benchi lilifikia uamuzi huo kutokana na wingi wa mashindano yanayowakabili, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf).
 

“Ukiangalia tuna michuano mingi ambayo inatulazimu kuwa na kikosi kipana zaidi. Caf, ligi kuu, Kombe la FA na hapohapo Mapinduzi inatusubiri siku chache zijazo.
“Hivyo kuna kila sababu ya kuwa na kikosi kipana, siyo kuwategemea wachezaji walewale (Donald) Ngoma na (Amissi) Tambwe, wakiumia je?
“Hivyo lazima uwe na kikosi kipana ili kama ni kasi ya kushambulia kusionekane pengo michuano kwa michuano,” alisema Mwambusi.

No comments:

Post a Comment

paulmkale