Pichani ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence
Milanzi ambaye leo ameapishwa rasmi kuanza kupambana na majangili ambao
wamekuwa kero kwa nchi hii.
Ikumbukwe kuwa kuna wakati Tanzania
ilifikia kuwa kinara cha matukio ya ujangili kiasi cha Serikali ya Awamu
ya Nne kuanzisha Operesheni Tokomeza ambayo nayo haikuisha vizuri.
Maliasili
ya Tanzania ikitunzwa vizuri inaweza kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa
nchi ambayo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi
kupitia utalii.
Tunakutakia kila la heri katika majukumu yako mapya Meja Jenerali Gaudence Milanzi.

No comments:
Post a Comment
paulmkale