Mbwana
Samatta akipokelewa uwanja wa ndege usiku wa kuamkia leo mara baada ya
kuwasili akitokea Nigeria, mwenye suti ni Baba mzazi wa Mbwana Samatta,
Mzee Samatta. Aliwasili usiku huo akitokea Nigeria kwenye tukio la
utoaji wa tuzo za mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka 2015 . Mbwana
alifika katika uwanja huo wa JNIA majira ya saa nane usiku.
Na Andrew Chale,Modewjiblog
Tuna kila
sababu ya kujivunia Mbwana Samatta kama alama ya Tanzania. Hata hivyo
tayari kumekuwa na hali ya kutoeleweka kwa sasa dhidi ya taarifa tata
zikiwemo zile za mitandao ya nje kumtambulisha Mbwana Samatta kama raia
wa Congo pia wapo walioandika Mbwana Samatta raia wa Tunisia na nchi
zingine, lakini pia hata mitandao mingine kushindwa hata kumtaja kama
anatokea Tanzania.
Hata
hivyo hali hiyo iliamsha hasira za haraka kwa mashabiki na watanzania
wengi ambao walichukizwa kwa kushindwa kumtambulisha vyema Mbwana
Samatta. Lakini hilo sio ‘issue’ kubwa sana ila kuna hili la ujio wake
wa usiku wa manane.
Shujaa
wetu wa Afrika, Mbwana Samatta ameweza kuwasili nchini salama kabisa
hilo la kumshukuru Mungu. Hata hivyo wengi wa watanzania kupitia
mitandao ya kijamii wamelalamikia ujio wake huo wa usiku wa manane
wakikosa nafasi ya kumpokea kwa wingi kama wafanyavyo mashujaa wengine
wanapowasili kwenye viwanja vya ndege.
Hilo la
ujio wa usiku wa manane tusiumize sana vichwa huenda ndio ratiba sahihi
ya ndege licha ya watu kudai kuwa TFF ama serikali ilikuwa na uwezo wa
kumbadilishia ndege na akaingia mapema ziadi ya hapo lakini yote kwa
yote shujaa wetu amefika salama na amekuja Tanzania na sio Congo ama
Tunisia ama huko wanakosema wengine ambao hawamjui vyema Mbwana Samatta.
Kuna hili
la kutokuwapo viongozi wakubwa wa Kiserikali wakiwemo waziri ama Katibu
mwenye dhamana kushindwa kutokea uwanja wa ndege najua hilo ni tatizo
kwa baadhi ya wananchi waliolalamikia hilo hasa wale waliofika uwanja wa
ndege huku kwenye mitandao ya kijamii kukiwa na gumzo kwa nini
hawakufika kumpokea ?…. Ok Karibu nyumbani Mbwana Samatta.
Mbwana
Samatta akipata picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari
waliofika kumpokea. Katikati aliyeshika tuzo hiyo ya Mbwana Samatta,
Mhariri wa Tanzania Daima, Tullo Chambo akipata picha ya ukumbusho.
Baadhi wanahabari wa New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba na Sport Starehe wakipata picha ya ukumbusho na Mbwana Samatta.
No comments:
Post a Comment
paulmkale