Waziri wa
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akiwa katika
picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na
Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari mapema leo, alipokutana
nao na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri tasnia hiyo,mkutano
huo umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini
Dar.
Mh.
Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara
ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Mh. Nape
Nnauye akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo
pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano uliohusu kujadili mambo
mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabiri tasnia ya habari hapa
nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda
na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi
Kawawa .
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha
Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani), mapema leo jijini Dar,
kwenye mkutano ulioitishwa na Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo
mbalimbali yanayoikabiri tasnia ya habari hapa nchini. Pichani katikati
ni Waziri Mh. Nape pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom
Kibanda.(P.T)
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa
Vyombo vya habari (hawapo nchini) kuhusina na mkutano wao ulioitishwa na
Waziri Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabiri
tasnia hiyo kwa ujumla.
Baadhi ya
Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo
wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.
Mmoja wa Wahariri Kurwa Kaledia kutoka New Habari Hause akiomba ufafanuzi wa jambo kwa Mh Waziri Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa makini.
Mmoja wa Wahariri Grace Hoka akifafanua jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Wahariri wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo.
Mmoja wa Wahariri akifafanua jambo kwenye mkutano huo
No comments:
Post a Comment
paulmkale