Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na viongozi
wa machinjio ya Vingunguti – Dar mara baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza usiku wa kuamkia leo.
…akipewa maelekezo
…akikagua machinjio hayo.(P.T)
Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, amemfukuza kazi
mkuu wa mnada wa mifugo wa Pugu, na watumishi walioshiriki kuiba ushuru
wa serikali, alipoenda machinjioni hapo kukagua.
Waziri
Nchemba amesema alienda machinjioni hapo kutatua kero zinazowakabili
wananchi na wadau wa machinjio hayo, huku akishirikisha wizara mbili ya
Afya na TAMISEMI.
“Nimerejea
asubuhi ya leo kwenye machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero
zinazowakabili watumiaji wa machinjio hayo, kutokana na uwepo wa
ubadhilifu wa kodi ya serikali kwenye mnada wa pugu na malalamiko kadhaa
yanayogusa wananchi wanaotumia machinjio haya, nimeshirikisha wizara
mbili (TAMISEMI na AFYA) kutoa majawabu ya muda mfupi na ya
kudumu”, alisema Waziri Nchemba
Baada ya
kufika machinjioni hapo Waziri Mwigulu Nchemba alitoa maagizo kwamba
Mkuu wa mnada wa machinjioni hapo watafute kazi nyingine, na kuwataka
kufika ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara.
“Nimeagiza
kuwa Mkuu wa mnada wa Pugu na watumishi waliokuwa zamu tar. 24.12.2015
na tar.01.01.2016, kuanzia sasa watafute kazi nyigine, wakati huohuo
wahakikishe wanafika ofisi ya Katibu mkuu wizarani kwangu mapema
Jumatatu tar.04/01/2016”, alisema Waziri Nchemba.
Pamoja na
hayo Waziri Nchemba amesitisha uchukuaji wa ushuru katika eneo la mnada
wa Pugu, na kutaka makusanyo ya fedha zote yafanyike machinjio ya
Vingunguti kwa kutumia mashine za EFD.
“Kuanzia
sasa nimesitisha uchukuaji wa ushuru eneo la mnada wa Pugu, badala yake
makusanyo yote ya fedha za serikali yatafanyika machinjio ya Vingunguti
kwa kutumia mashine za elektroniki za EFD, kwa maana hiyo mnada wa Pugu
utakuwa unatumika kutoa vibali tu vya mifugo ilikudhibiti ubora wa
mifugo inayopaswa kuchinjw”, alisema Waziri Nchemba.
Pia
waziri Nchemba ametaka eneo la kuhifadhia nyama lililokuwa limejengwa
kwa fedha za wananchi kushirikiana na serikali lifunguliwe kwa ajili ya
wananchi kulitumia kuhifadhia nyama.
Hatua za
kuboresha miundombinu ya machinjio hayo zimeelekezwa kwa Halmashauri ya
Ilala zifanyiwe kazi haraka na kwa ubora, na kutakiwa kurudishwa kwa
umeme uliokuwa umekatwa eneo hilo, kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi
shughuli zao.
No comments:
Post a Comment
paulmkale