Waziri wa mambo ya ndani wa Saudi arabia, Mansour al-Turki katika mkutano na waandishi wa habari mjini Riyadh, Januari 2, 2016.
Na RFI
Saudi
Arabia imewanyonga watu 47 Jumamosi hii waliohukumiwa kwa kosa la
"ugaidi", ikiwa ni pamoja na kiongozi wa kidini kutoka jamii ya Mashia,
Nimr Baqir al-Nimr, kiongozi wa kundi linaloipinga serikali ya nchi
hiyo.
Hali hiyo imezua hasira katika jamii ya Mashia ulimwenguni.
Miongoni
mwa watu wengine 46 walionyongwa ni pamoja na wanajihadi wengi wa Al
Qaeda, wakati ambapo utawala wa kifalme una wasiwasi kuhusu tishio la
Masuni wenye msimamo mkali kama kundi la Islamic State (IS). Kundi la Al
Qaeda hivi karibuni liliapa kulipiza kisasi iwapo wanamgambo wake
watanyongwa.
Iran
imeghadhabishwa na kitendo hicho cha kuuawa kwa Cheick al-Nimr.
Mahusiano wakati huu kati ya Iran yenye Mashia wengi na Saudi Arabia
yenye Masuni wengi yamedorora kwa kiasi kikubwa. Tehran imeionya Riyadh
kuwa itajutia kifo hicho, wakati ambapo maandamano yameitishwa nchini
Iran kufanyika Jumapili dhidi ya Saudi Arabia.
Picha ya
kiongozi wa kidini kutoka jamii ya Mashia Nimr al-Nimr ikichikiliwa na
mmoja wa waandamanaji Oktoba 18, 2014 mbele ya ubalozi wa Saudi katika
mji wa Sanaa wakipinga adhabu ya kifo dhidi ya kiongozi wa upinzani.(P.T)
Akiyakosoa
maeneno ya serikali ya Tehran, msemaji wa Wizara ya mambo ya ndani ya
Saudi Arabia, Mansour al-Turki, amesema nchi yake "haitishwi na fikra za
wengine."
Watu
walionyongwa, ikiwa ni pamoja na raia 45 wa Saudi Arabia, raia mmoja
kutoka Misr na mmoja kutoka Chad wameuawa kwa upanga au kwa kupigwa
risasi katika miji kumi na miwili ya Saudi Arabia.
Walikuwa
wamehukumiwa, kwa mujibu wa serikali ya Saudi Arabia, katika kesi
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujiunga na itikadi yenye msimamo mkali,
kutoka "makundi ya kigaidi".
Tawala za
kifalme kutoka jamii ya Masuni katika Ukanda huo, ikiwa ni pamoja na
Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu zimekaribisha mtizamo wa Saudi
Arabia. Nchini Bahrain, baadhi ya vijana wa Kishia walio wengi, hata
hivyo, wamekusanyika katika kitongoji cha Manama kupinga mauaji hayo.
Sheikh Nimr al-Nimr, amenyongwa nchini Saudi Arabia, alikuwa mpinzani mkuu wa utawala wa kifalme nchini humo
No comments:
Post a Comment
paulmkale