Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
akizungumza na wadau mbalimbali juu ya kufanisha uzinduzi wa Stika
maalumu yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo
jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Stika maalumu yenye ujumbe wa
kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism jijini Dar es Salaam,kulia ni
Mwenyekiti wa Albno Enteprises of Dar es Salaam Michael Lugendo.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
akupokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Albino kutoka Enteprises of Dar
es Salaam, Michael Lugendo leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
akionesha Stika mara baada ya uzinduzi wa wa Stika maalum yenye ujumbe
wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi waliofika katika uzinduzi wa
Stika maalum yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye
Albinism,leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Kanda Maalimu ya Dar es
Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)
KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
leo amezindua stika za kutokomeza mauaji kwa watu wenye albinism.
Kamanda
Sirro amesema lengo la stika hizo ni kutoa elimu maeneo yote hasa
katika mikoa ya Kanda ya ziwa ambapo mauaji ya albino yamekithiri.
Amesema
stika hizo zitasambazwa nchi nzima kwasababu ipo mikoa mbalimbali bado
ina mila potofu za kishirikina ambapo watu wanaamini kuwa akipata viungo
vya albino atakuwa tajiri.
Amesema
kuwa kusudi ni kutotoa elimu kwa njia ya stika ni kwamba zitabandikwa
katika majumba, maofisini, kwnye magari, madukani, mashuleni, vyuoni,
kwenye bodaboda na bajaji na elimu hiyo itamfikia hata yule mtanzania
ambaye hana redio na runinga.
“Tuna kila sababu kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa amani na kuwalinda ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi(Albino.
“Sisi
kama jeshi la Polisi na vyombo mbalimbali vya dola tunawajibika kupata
taarifa za wale wanaotafuta viungo vya albino tutahakikisha tunapata
taarifa kabla ya tukio halijafanyika,” alisema Kamanda Sirro.
Amesema
jeshi hilo litashirikiana na Viongozi wa Serikali za mtaa, viongozi wa
dini zote pamoja na taasisi mbalimbali zenye kutetea haki za binadamu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya AlbinoInterprises Dar es Salaam,
Michael Lugendo, alisema lengo la stika hizo ni kutokomeza mauaji lwa
watu wenye albinism na kazi hiyo inahitaji ushirikishwaji wa kila mtu.
Amesema
hapa nchini albino wanakabiliwa na mauaji ya aina tatu ambayo ni mauaji
ya kisaikolojia yanayomgusa kila mtu mwenye albinism ambayo yalianza
pale vitendo vya kukata viungo vya albino vilipoibuka.
Kugendo
amesema mauaji mengine ni yale yanayosababishwa na saratani ya ngozi
ambayo hutokana na ukosefu wa mafuta ya ngozi na vikingia jua kulingana
na mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na mauaji ya kukatwa viungo ambavyo
jamii jamii kubwa inawatambua hadi sasa wanaofanya vitendo hivyo.
Hata
hivyo aliwataka viongozi wa dini, wanasiasa, wafanyabiashara kuwasaidia
michango ili kuwezesha zoezizima la usambazaji stika hizo.
Pia
taasisi hiyo ilimtunuku Kamanda Sirro tuzo ya amani na upendo pamoja na
kutoa cheti cha kujali jamii kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF).
Kamanda
Sirro amesema kuwa tuzo hiyo ni mwanzo mzuri kwake na ina mpa moyo wa
kuendelea kushirikiana na albino katika kutokomeza mauaji.
No comments:
Post a Comment
paulmkale