Inawezekana umemuona mwimbaji staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz
akiwa kwenye maisha mazuri kuanzia nyumbani kwake mpaka usafiri
anaotembelea ila hujajua kwamba amekua akifanya ibada na kumshukuru
Mwenyenzi Mungu.
Diamond Amesema, “Msikiti nimeujenga kule Mkuyuni Morogoro ni baada
ya boss wangu Tale kuniambia kwamba kuna msikiti kule Mkuyuni na watu
wanaswali kwa tabu sababu Msikiti ni wa udongo, watu wanapata tabu.”
Diamond akaongezea, “Tuliuvunja mpaka tukaanza mwanzo kuujenga, sasa
hivi ulipofikia ni karibia kukamilika…. gharama yake mpaka kukamilika ni
zaidi ya milioni 30.”
Akaendelea, “Mwaka 2015 nilijitahidi kufanya vitu vingi vya dizaini
hii Mwenyenzi Mungu aone kabisa inawezekana kazi yangu ya muziki sio
nzuri ila natumia kufanya mambo ya msingi.”
No comments:
Post a Comment
paulmkale