Diamond na Jah Prayzah wa Zimbabwe washoot video ya collabo yao SA

Baada tu ya kutoka kurekodi collabo ya Coke Studio ZA na Cassper Nyovest, Diamond Platnumz aliingia location kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na staa wa Zimbabwe, Jah Prayzah.Jah 1
Prayzah ambaye jina lake halisi ni Mukudzei Mukombe alilazimika kusafiri hadi Dar es Salaam kuja kukamilisha collabo yake na Diamond hivi karibuni.
Jah Prayzah ambaye hujulikana pia kwa jina la Musoja kutokana na kupenda kuvaa nguo za kijeshi, amemshirikisha Diamond kwenye wimbo wake uitwao Watora Mari.
Wimbo huo utapatikana kwenye album yake mpya na ya saba, iitwayo Mudhara Vachauya itakayozinduliwa August 12.
Diamond ameshare picha Instagram akiwa na staa huyo na kuandika: Wraping it up my Zimbabwean brother @jahprayzah Video #Kidogo before spending time with my Miss world!”Jah 2Jah Prayzah naye ameshare video akiwa na Diamond kuelezea ujio wa video yao.

No comments:

Post a Comment

paulmkale