Meneja wa Diamond, Babu Tale ameonyesha kuwa wao hawana tatizo na Alikiba baada ya kupost kipande cha video kinachoonyesha picha ya msanii huyo ndani ya studio ya Wasafi Records.
Ni muda mrefu imezungumzwa kuwa Diamond platnumz na Ali kiba
wana bifu mpaka kupelekea kuanzishwa kwa baadhi ya team za mitandaoni
za kukejeli mafanikio ya msanii wa team nyingine lakini hiyo ni dalili
kuwa ipo siku itabaki historia tu.
Babu Tale alipost kipande hicho cha video kinachoonyesha baadhi ya picha za wasanii wakubwa Bongo akiwemo Marehemu Bi Kidude, Mr Blue, Dully Sykes, Juma Nature, Q Chief, Ali kiba na wengine wengi.
Je, hiyo inaweza ikawa ndiyo kiki ya kuikaribisha video ya wimbo mpya wa Diamond aliowashirikisha P Square ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni?
Tazama video hapa.
No comments:
Post a Comment
paulmkale