ARSENAL YAMUONGEZEA KIUNGO WAKE MKATABA WA MUDA MREFU MPAKA 2023


Kiungo wa klabu ya Arsenal, Granit Xhaka amesaini mkataba wa muda mrefu na timu hiyo utakaomuwezesha kuendelea kusalia mpaka msimu wa 2022/23.

Mswizi uyo ameaminiwa na kocha mpya wa timu hiyo aliyechukua mikoba ya muda mrefu, Unai Emery, akirithi nafasi ya Arsene Wenger aliyeitumikia Arsenal kwa muda mrefu.

Emery amesema kuwa amefurahia kwa kiungo huyo kuongeza mkataba mwingine na Arsenal kutokana na umuhimu wake ndano ya dimba.

Aidha, Emery amefunguka na kusema uwepo wa Xhaka kwa muda mrefu na umri alionao utamfanya kuzidi kuimarika zaidi na zaidi kama kizazi kijacho.

No comments:

Post a Comment

paulmkale