RONALDO NA REKODI ZAKE ZA JANA, MESSI NAYE HUYU HAPA LEO
Na George Mganga
Cristiano Ronaldo jana alifanikiwa kufunga mabao matatu pekee 'Hat-trick' katika mchezo wake wa kwanza wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu dhidi ya Spain nchini Urusi.
Mabao hayo yaliisaidia Ureno kwenda sare ya 3-3 dhidi ya mabingwa hao wa Kombe la Dunia kwa mwaka 2010 huko Afrika Kusini.
Hattrick hiyo imekuwa ya 51 kwa Ronaldo katika soka la ushindani huku akiifunga akiwa na umri wa miaka 33, moja ya wachezaji wenye umri mkubwa katika mashindano hayo.
Rekodi hizo kadhaa za Ronaldo zinamfanya Messi ambaye hajawahi kutwaa ubingwa wa taji hilo kujipanga kwa ajili ya kulipiza mapigo.
Mara nyingi wawili hawa wakiwa viwanjani wamekuwa ni watu wa kuvunja na kuandika rekodi za aina yake na kipekee.
Messi atakuwa anashuka dimbani kuingoza Argentina kucheza kibarua chake cha kwanza leo dhidi ya Iceland.
Pengine anaweza akajibu kwa kufunga pia mabao kama aliyofunga mpinzani wake ingawa huu ni mchezo wa soka mambo yanaweza kuwa tofauti.
Tusubiri tuone namna gani Lapulga amejipanga kuelekea mechi hiyo ambayo Argentina watakuwa wanafungua pazia lao kwenye michuano hii.
Messi na Ronaldo wote kwa uwili wao hawajawahi kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia wakiwa na timu zao za taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
paulmkale