YAANZA KUFANYA KAZI YA KUSAKA BEKI WA KATI, NI NDANI NA NJE YA TANZANIA




Kikosi cha mabingwa wa Tanzania, Simba taratibu kimeanza kusaka beki wa kati.

Taarifa zinaeleza, Simba imeanza zoezi hilo ndani na nje ya Tanzania kuhakikisha inapata beki wa uhakika wa kati.

“Kazi imeanza, wanapitia CV mbalimbali lakini leo ni kupata beki wa uhakika ambaye ataaminika.


“Unajua Simba ina mabeki wazuri lakini ugumu wa mashindano tunayokwenda nao una shida yake. Hivyo kazi inaendelea kwa utaratibu sahihi,” kilieleza chanzo.


Inaonekana kama mabeki wa Simba hasa Yusuf Mlipili wamekuwa wakipata kazi ngumu katika michuano ya kimataifa kutokana na uzoefu.

Ndani ya Simba kumekuwa na majadala kuhusiana na kubaki au kuachwa kwa beki Juuko Murshid ambaye inaonekana Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre hakumkubali kabisa.

No comments:

Post a Comment

paulmkale