Showing posts with label JUX. Show all posts
Showing posts with label JUX. Show all posts

Juma Jux: Nilimpenda Jackie Cliff ila Sitarudiana Nae Tena, Nina Maisha Mapya.

Msanii Jux ambaye kwa sasa yupo kimahusiano na Vanessa Mdee, amefunguka na kuweka wazi sakata ambalo lilimkuta mpenzi wake wa zamani anayefahamika kama Jackie Cliff na mahusiano yake na model huyo.

Kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa na EATV Jux alikiri wazi kuwa alikuwa akitoka kimapenzi na Jackie Cliff na kusema alikuwa anampenda sana licha ya bidada huyo kumzidi umri.
Jux alidai katika kipindi chote ambacho wapo katika mahusiano hakuwahi kutambua wala kuhisi kama Jackie Cliff alikuwa akijihusisha na biashara ya dawa za kulevya mpaka siku alipopata taarifa kuwa amekamatwa ndipo alipojua suala hilo.

“Kiukweli nilimpenda sana Jackie Cliff maana mara nyingi mimi napokuwa na mtu huwa napenda kweli sababu huwa nahitaji kutulia, lakini huwezi amini sikuwahi kutambua kama Jackie Cliff anafanya mambo hayo mpaka alipopata matatizo hayo ndiyo najua mimi, hivyo ilinipa wakati mgumu sana mimi kiasi kwamba nilikuwa sijielewi”. Alisema Jux

Jux aliendelea kudai kuwa wakati Jackie Cliff anapata matatizo hayo yeye alikuwa amekuja likizo Tanzania hivyo ndiyo siku hiyo hiyo ‘Producer’ wake Manecky alipompigia simu na kumwambia aende studio na kumwambia anapaswa kufanya kitu ndipo hapo alianza kuandika na kufanya wimbo wa ‘Nitasubiri’ ambao anadai walishirikiana na watu wengine studio kuutengeneza na kuandika baadhi ya mashairi kwenye wimbo ule ambao ulikuwa maalum kwake.

“Huwezi amini siku ambayo Jackie alipata matatizo Manecky alinipigia simu na kuniambia njoo studio, nilipofika pale akaniambia lazima tufanye kitu ndiyo tukaanza kuandika na kutengeneza wimbo ule, lakini ikitokea ametoka saizi Jackie Cliff sitaweza kuwa naye tena sababu tayari nishaanza maisha mapya” alidai Jux.

Jux : Usikubali kuombwa hela kwenye Mitandao kupitia jina Langu

Jux ameamu kutoa tarifa kwa mashabiki zake kuhusu watu wanao fungua page na kutumia jina lake, ameamua kundika  post katika page yake ya Facebook ili kuweza kuwa kuwapa tahadhari kuogopa watu wasije kutapeliwa n.k .

Kupitia mtandao wa facebook Jux ameandika:
"Inakuwaje watu wangu kumekuwepo na accounts nyingi humu facebook ambazo zimekuwa zikitumia jina langu kutapeli watu! Please naomba mjue sina account/page yeyote humu FB zaidi ya hii page tu!
Usikubali kuombwa hela(kutapeliwa) kupitia jina langu!
"

Jux Ampoteza Diamond Platnumz Kwa Mjengo Wenye Hadhi ya Kistaa


Juma JuxKwa muda mrefu kumekuwa na Habari nyingi zisizo na uhakika kuhusu nyumba anayomiliki Mwanamuziki Diamond na huku wengine wakilaumu kwa yeye kuendelea kukaa nyumba ya kupanga kulinganisha na mafanikio yake kimuziki... Mwanmuziki Jux ambae umaarufu wake si wa kiivyo katika muziki anaonekana kumpoteza kabisa Diamond kutokana na Hekalu analomalizia kujenga lenye ghorofa moja... Jumba hilo lenye hadhi ya kistaa lina studio ya kurekodi, Gym kwa ajili ya mazoezi na Bwawa la Kuogelea ndani....

Jux, Nahreel na Iyanya waingia gym kupasha, ni collabo mpya?

Mwaka huu Jux ana spidi kali. Baada ya kutoka kushoot video ya wimbo aliomshirikisha Joh Makini (haujatoka) nchini Afrika Kusini, muimbaji huyo huenda akawa anatengeneza collabo na msanii wa Nigeria, Iyanya. Muimbaji huyo ambaye wiki iliyopita aliachia video ya wimbo wake mpya ‘Nikuite Nani’ amepost picha akiwa na Iyanya na producer Nahreel.

Kaa Tayari;Ujio mpya "NIKUITE NANI?ni Juma tano hapa hapa

Wewe ungependa uitwe nani?Ungana nami

Paulmkale.blogspot.com

kusuilia kitu hiki kutoka kwa mkali wetu

Picha,Huu ndo mjengo wa gorofa wa msanii Jux, anakuambia #Donewitchildishdreams.

Baada ya Jux kupost picha ya nyumba yake Jux alionyesha furaha yake akitamani kuhamia baada ya kutimiza ndoto zake.
Kwenye picha aliyoweka instagram, iliambatana na ujumbe uliosema
” Done with childish dreams on to bigger things #africanboy #inGoditrust #icantwait #soon ”