Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itawasomea maelezo ya awali (PH) na kuanza rasmi kuisikiliza kesi ya jinai inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa siku tano mfululizo, kuanzia Juni 25 hadi 29, 2018.
Mbowe na wenzake walipaswa kusomewa maelezo ya awali leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri lakini ilishindikana kwa sababu mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Freeman Mbowe amefiwa na kaka yake Henry Mbowe na amekwenda msibani, Moshi.
Pia, Mahakama imemtaka mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo, Esther Matiko mbunge wa Tarime mjini ambaye ni mgonjwa ahudhurie mahakamani bila ya kukosa na asipofanya hivyo hatua dhidi yake zitachukuliwa.
Hata hivyo, mawakili wanaowatetea washtakiwa hao Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya hawakuwapo mahakamani, Kibatala alikuwa amehudhuria kesi Mahakama Kuu, huku Mtobesy, akihudhuria kesi Mahakama ya Afrika Mashariki Arusha.
Hivyo waliwakilishwa mahakamani hapo na mawakili Nashon Nkungu, Frederick Kihwelo na Hekima Mwesigwa.
Awali, wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alieleza mbele ya Hakimu Mashauri kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa Maelezo ya awali na kwamba wamejipanga kuendelea.
Lakini ilishindikana kwa sababu Mshtakiwa
Mbowe hakuwapo mahakamani kwa sababu amefiwa na kaka yake Henry Mbowe na amekwenda Moshi katika mazishi.
Mbowe aliwakilishwa mahakamani hapo na mdhamini wake Grayson Celestine ambaye aliwasilisha nakala ya cheti cha kifo mahakamani ili kuithibitishia Mahakama.
Kwa upande wa mshtakiwa Esther Matiko aliwakilishwa na mdhamini wake, Patrick John aliyeieleza Mahakama kuwa anaumwa na akawasilisha nyaraka ya mapumziko kutoka kituo cha afya.
Hata hivyo, nyaraka hiyo ilipingwa na wakili Nchimbi kwa madai kuwa ni batili haina Maelezo yanayojitosheleza ambayo yanayoweza kuishawishi mahakama kuamini Matiko ni mgonjwa na anapaswa kupumzika kwa siku saba.
Washtakiwa waliokuwapo mahakamani ni mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu Bara na John Mnyika.
Katibu wa chama hicho, Dk Vicenti Mashinji, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo kufanya mkusanyiko usio halali, na kusababisha ghasia. Pia wanadaiwa Februari mwaka huu walikiuka agizo la kuwataka kutawanyika na kusababisha uvunjifu wa amani.
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Breaking News: Dr. Ali Mohammed Shein Atangazwa Rasmi kuwa Mshindi wa Kiti Cha Urais Zanzibar Kwa Asilimia 91.4
ACT Wazalendo Chamvua Uanachama Ofisa Mipango Na Aliyekuwa Mgombea Urais Zanzibar
Chama cha ACT Wazalendo kimemsimamisha uanachama Ofisa Mipango wake, Ali
Makame Issa kwa madai ya kukiuka maadili ya chama hicho.
Hata hivyo, Issa alisema jana kuwa hajapokea taarifa yoyote kutoka katika chama hicho.
Hatua
hiyo dhidi ya kiongozi huyo mwandamizi ndani ya ACT, imekuja baada ya
chama hicho kudai kuwa alishirikiana na aliyekuwa mgombea wa urais wa
Zanzibar, Khamis Iddi Lila kuwahujumu.
Awali, Lila alisimamishwa
uanachama kwa madai ya kutoa misimamo ya kushiriki uchaguzi wa marudio
uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha
Salim Jecha.
Barua ya ACT, iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa
chama hicho, Juma Said Sanani imesema: “Kamati maalumu ya Zanzibar
imekusimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11
(2) kuanzia leo Februari 19, 2016, kwa ukiukwaji mkubwa wa
katiba Ibara ya 7 (3)(5)(9) Ibara ya 10 (2)(c) (d), Ibara ya 22 (1) (2)
(4).”
Barua hiyo inabainisha kuwa mwanachama huyo amekiuka kanuni na maadili pamoja na kukidhalilisha chama.
“Huku
ni kukiingiza chama katika mgogoro kwa kuandika barua ya kushiriki
uchaguzi wa marudio na kuhudhuria katika kikao cha Tume ya Uchaguzi
Februari 17 ukijua kuwa chama kimeshapeleka barua Febuari 9 ya
kutoshiriki uchaguzi,” inaeleza.
Vyama vilivyowachukulia hatua
viongozi wake kwa madai ya kukiuka kanuni ni Sauti ya Umma (SAU),
kilichomfukuza aliyekuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Issa Mohamed
Zonga, huku Alliance for Democratic Changes (ADC) kikimfukuza aliyekuwa
mlezi wake, Hamad Rashid Mohamed
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA MAKUNDI YALIYOSHIRIKI NAYE KWENYE KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015
Waziri
Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe
Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni
ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es
salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia katika mkutano wa Rais
John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye
kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu
jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Rais
John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki
naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru
Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Rais
John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki
naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru
Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Rais
John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na kundi la sanaa la
Tanzania One Theatre baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki
naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru
Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016
Rais
John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wataalamu wa
TEHAMA baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye
kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini
Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016
Rais
John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo
Fleva baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye
kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini
Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Rais
John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo
Movie baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye
kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu
jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Rais
John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na sehemu ya
wanahabari aliokuwa nao katika kampeni baada ya kuongea na baadhi ya
makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015
aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February
18, 2016
Rais
John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na watendaji kutoka
CCM Makao Makuu baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki
naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru
Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Rais
John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mhe January Makamba huku Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye kabla ya kuongea
na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi
mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo
Alhamisi February 18, 2016.
Rais
John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli wakiongozana na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe
January Makamba huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe
Nape Nnauye wakielekea ukumbini kuongea na baadhi ya makundi
yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita
kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016
PICHA NA IKULU
Mbowe Aanza Kulisuka Baraka Kivuli La Mawaziri

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametoa mwelekeo wa upangaji wa uongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni na baraza kivuli la mawaziri, huku akionyesha kambi hiyo kuwa tayari kushirikiana na Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
Akizungumza
jana mjini Dodoma Mbowe alisema idadi ya wizara hizo itafanana na ya
wizara za Serikali ya Awamu ya Tano ambazo zipo 19.
“Tutatangaza
baraza kivuli kabla ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge Ijumaa wiki hii
na baraza hili litashirikisha vyama vyote vinavyounda Ukawa,” alisema Mbowe.
Alisema
kigezo cha kwanza kitakuwa uzoefu na taaluma za wabunge kikifuatiwa na
mgawanyo wa nafasi kwa kuzingatia kipaumbele hicho kwanza.
“Tutazipanga
kulingana na muundo wa Muungano kwa sababu kuna wizara ambazo ni sehemu
ya Muungano. Nne tutazingatia jinsia kadri iwezekanavyo na tano
tutazingatia uteuzi kulingana na mikoa, yaani mawaziri vivuli
watateuliwa kulingana na mikoa wanayotoka kadri itakavyowezekana.”
Alisema
miaka yote, upinzani ulikuwa ukiitaka Serikali kupunguza ukubwa wa
Baraza la Mawaziri, hivyo uamuzi wa Rais John Magufuli kupunguza idadi
ya wizara ni jambo zuri na wao watafanya hivyo katika uteuzi wa baraza
hilo kivuli.
Kuhusu Zitto alisema:
“Katika siasa na ushirikiano wa vyama hakuna mazingira ya kudumu. Jambo
lolote linawezekana lakini kuna taratibu zake na muda ndiyo huwa
unaongea.”
Alisema
Chadema na NCCR vimewahi kuwa na wabunge ambao kwa sasa ni makada wa
CCM, huku akitolea mfano jinsi Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa
alivyohama CCM na kujiunga na Chadema na kugombea urais.
“Hatujawahi
kama kambi ya upinzani kumtenga Zitto kwenye kila jambo, yapo mambo
tunaweza kulazimika kutengeneza ushirikiano na wabunge hata wa CCM ili
kufanya jambo fulani kutekelezeka.
“Kushirikiana
na Zitto si jambo la ajabu kama ambavyo umeona tukilifanya. Yapo
majeraha mengi ambayo tumeyapitia pande zote (Chadema na Zitto) ambayo
huwezi kuyatibu kwa siku moja.
"Yapo
ambayo yatapona kulingana na muda. Unaweza kumfanyia mtu kitu kibaya,
lakini baadaye ukatambua kuwa umekosea. Chochote katika siasa
kinawezekana,” alisema Mbowe.
Zitto
alifukuzwa Chadema na kujiunga na ACT Wazalendo Machi 21, 2015 chama
ambacho hakina ushirikiano na vyama vinavyounda Ukawa lakini katika siku
za karibuni ameonekana kuwa karibu na umoja huo wa wananchi, ikiwa ni
pamoja na kushirikiana kuibua hoja mbalimbali katika mkutano wa Bunge
unaoendelea mjini Dodoma.
Viongozi wa UKAWA Kutoa Msimamo Wao Juu ya Suala la Zanzibar

UMOJA
wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema utatoa msimamo juu ya hali ya
siasa ya Zanzibar baada ya kikao cha kamati tendaji kuketi na kutoa
msimamo. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema
hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Alisema
walifanya mazungumzo ya mashauriano ya hali ya siasa ya Zanzibar,
yaliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa nyama vya upinzani,
wakiongozwa na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF,
Maalim Seif Shariff Hamad na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward
Lowasa.
“Januari
28 keshokutwa kutakuwa na kamati ya utendaji na kikao hicho, kitatoa
msimamo wa kitu gani kifanyike kuhusiana na siasa za Zanzibar,” alisema. Pia, alisema Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), litatoa msimamo wake kuhusu suala la Zanzibar.
Mbunge
wa Malindi kwa tiketi ya CUF, Ally Salehe alisema wanaamini Rais John
Magufuli, anaweza kuingilia mgogoro wa Zanzibar na kuupatia ufumbuzi.
Andrew Chenge Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa Bunge
MBUNGE
wa Bariadi, Andrew Chenge na wabunge wawili wa Viti Maalumu, Dk Mary
Mwanjelwa na Najma Giga, wamechaguliwa kuwa Wenyeviti wa Bunge kwa
kipindi cha miaka miwili na nusu.
Uchaguzi
huo ulifanyika jana baada ya majina yao kupendekezwa na Kamati ya
Uongozi na kuyawasilisha bungeni kwa ajili ya uchaguzi.
Katika
uchaguzi huo, uliotanguliwa na wabunge hao kujieleza mbele ya wenzao na
kuulizwa maswali, sakata la Tegeta Escrow liliibuka baada ya Chenge
kujieleza.
“Katika
Bunge lililopita, chama chako na wabunge walikuwajibisha kwa kashfa ya
Escrow, je, siku ukiliongoza Bunge na hoja ikarudi ndani uko tayari
kuisimamia,” Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema) alimuuliza Chenge.
Akijibu
swali hilo, Chenge alisema Bunge linaongozwa na Kanuni na itakapokuja
mbele ya Bunge au kwenye Kamati, ikaonekana kuna maslahi ama inamhusu
mbunge, ni busara kuzingatia kanuni nafasi hiyo ikaachwa mwingine
aifanye shughuli za Bunge zisiwe na makandokando ya aina yoyote.
“Naona niishie hapo, ningeweza kusema zaidi ya hapo,”
alisema Chenge ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa zaidi ya
miaka 10 na pia Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la 10 kabla ya
kujiuzulu kutokana na sakata la Tegeta Escrow.
Awali akijieleza Chenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, alisema “napenda niliahidi Bunge na Watanzania kwa ujumla, kwamba hii ni dhamana nzito ya kumsaidia Spika na Naibu.
“Lakini
niwahakikishie nitatekeleza jukumu hilo kwa uadilifu, na kwa uaminifu
ili nitende haki inayoonekana na bila chuki, wala upendeleo wowote kwa
faida ya kujenga misingi bora ya Bunge hili lakini pia kwa kuwatumikia
Watanzania wote,” alisema.
Kuhusu
swali la Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo (CCM) aliyetaka kufahamu ni
namna gani Chenge atadhibiti matumizi ya lugha ya kuudhi au kudhalilisha
wengine, Chenge alisema Kanuni za Bunge kama zilivyo sheria za nchi,
zinakata pande zote kama ilivyo msumeno.
Alisema ikithibitika kwamba mbunge amekiuka kanuni, kiti kitazingatia baada ya kupima kauli na maelezo aliyotoa bungeni.
“Baada ya kupima, tuhakikishe kwamba tunayosema humu bungeni yawe ya kweli, kweli tupu yasiwe ya uongo,” alisisitiza.
Mwanjelwa
ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Mbeya, katika kujieleza mbele
ya wabunge, aliomba wamwamini na kuahidi kuwatumikia bila kujali itikadi
kwa faida ya wananchi wote.
Mwanjelwa alikiri kwamba Bunge hili lina changamoto nyingi, lakini atakachozingatia ni utaifa kwanza.
Najma,
ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, aliahidi kuwa msaada mkubwa kwa Spika.
Aliahidi kuwa atahakikisha anaweka maslahi ya taifa mbele kwa kutoa
haki sawa kwa wabunge wote bila kujali vyama vyao.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai alihoji kwa pamoja wanaoafiki mapendekezo ya
Kamati ya Uongozi, ndipo wabunge walio wengi wakaridhia Chenge,
Mwanjelwa na Najma wawe wenyeviti. Wenyeviti wa Bunge hufanya kazi
wakati ambao Spika au Naibu Spika wakiwa hawapo bungeni.
Katika
Bunge la 10, wenyeviti walikuwa Mussa Azzan Zungu, Kidawa Himid Saleh,
Lediana Mng’ong’o, Muhammed Seif Khatib, Sylvester Masele na Jenista
Mhagama.
Kwa
mujibu wa Ndugai, Kamati yau Uongozi imejiwekea utaratibu wa
kupendekeza majina na ilipokutana chini ya uenyekiti wa spika, iliamua
kuwapendekeza wabunge hao watatu ambao wote ni kutoka CCM.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MKUTANO WA WABUNGE

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wabunge, bungeni mjini
Dodoma Januari 22, 2016. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto
ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kahilillah
Wabunge, Jenista Mhagama wa Peramiho (kushoto) na January Makamba wakiteta katika mkutano wa wabunge, bungeni mjini Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerge Masaju akitoa mada katika mkutano w wabunge , bungeni mjini Dodoma Januari 22, 20167
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wabunge, bungeni mjini
Dodoma Januari 22, 2016. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto
ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kahilillah
Mkurugenzi
wa Shughuli za Bunge, Nenelwa Mwihambi akitoa mada katika mkutano wa
wabunge ulioongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, buneni mjini Dodoma
Januari 22, 2016. Watatu kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kulia ni
Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilillah
Spika
wa Bunge Job Ndugai akizungumza kumkaribisha Mwenyekiti wa Mkutano wa
Wabunge, Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kufungua mkutano huo bungeni mjini
Dodoma Januari 22, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas
Kashilillah.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki,
Joshua Nasari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 22, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akiongea na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua
Nasari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 22, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mafinga mjini Cosato
Chumi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 22, 2016. Picha na
Ofisi ya waziri Mkuu
Subscribe to:
Posts (Atom)















![[IMG]](https://fbcdn-sphotos-d-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xaf1/v/t1.0-9/1382310_947228958645686_1731493795799039304_n.jpg?oh=d3e886aa1fb01749e15dcfd90238aed3&oe=574030B2&__gda__=1463849420_d443ef9fb77fd548d693a3bfea63ce18)
![[IMG]](https://scontent-lhr3-1.xx.fbcdn.net/hphotos-xap1/v/t1.0-9/12644690_947228985312350_7427097976973733940_n.jpg?oh=4425fbeebf457b79973de84ba3e3fc19&oe=57489EFA)
![[IMG]](https://fbcdn-sphotos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xtl1/v/t1.0-9/12647220_947228908645691_6617505679874419886_n.jpg?oh=1e30b64742fa5aa9358b61b6163e2962&oe=57468F69&__gda__=1462836436_9529568cf9a678ab1d1c11a5df0196f7)








