Unaweza
kusema ilikuwa moja ya mechi ya upinzani kweli, lakini mwisho ni Azam
FC imepata bao moja na wapinzani wao wakubwa Yanga bao moja.
mechi
hiyo ya Kombe la Mapinduzi hatua ya makundi kwenye Uwanja wa Amaan mjini
Zanzibar, leo. ilikuwa na ushidani wa juu huku ikitawaliwa na ubabe wa
hapa na pale.
Azam
FC ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kipre Tchetche katika
dakika ya 56 baada ya mabeki wa Yanga kujipanga vibaya na mfungaji
akavunja mtego na kuuwahi mpira kabla ya kupiga shuti kali lililomzidi
Deo Munishi ‘Dida’.
Yanga
nao waliendelea kupambana na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika
dakika ya 82 kupitia kwa Donaldo Ngoma baada ya makosa ya kipa Aishi
Manula ambaye alidaka mpira na kuudondosha.
Bao la
Yanga lilipatikana dakika chache baada ya nahodha wa Azam FC, John
Bocco kulambwa kadi ya pili ya njano iliyozaa kadi nyekundu.
Kila
timu imecheza mechi ya pili, Azam FC ikifikisha pointi mbili baada ya
sare ya kwanza ya mabao 2-2 dhidi ya Mtobwa Sugar, huku Yanga ikifikisha
pointi 4 baada ya kuanza michuano hiyo kwa ushindi.
No comments:
Post a Comment
paulmkale