#BringBackOurWema: Diamond awajibu mashabiki wa Wema,’ mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa…’

diamond platinumz & wema sepetu
Baada ya mashabiki wa muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu kuazisha kampeni waliyoipa jina la #BringBackOurWema kwenye mtandao wa Instagram (Isome hapa), wakimshinikiza Diamond Platnumz amrudishe Wema katika maisha yake ya zamani na kumsaidia katika career yake ya filamu, hit maker huyo wa ‘Number 1’ amewajibu.Haya ndio majibu marefu ya Diamond kupitia akaunti yake ya Instagram ambayo baadae alifuta:

“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu… kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe…

Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi…. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi….ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!!

Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!….Mxieeeeeeeew!”

No comments:

Post a Comment

paulmkale