‘Mtoto wa Mama’ ya Zachaa f/ Diamond & Godzilla kutoka Jumatatu

Producer anayefahamika kwa kutayarisha hits kama ‘Kesho’ ya Diamond na ‘Pombe Yangu’ ya Madee, Zachaa anatarajia kuachia wimbo wake ‘Mtoto wa Mama’ aliowashirikisha Diamond na Godzilla, Jumatatu ijayo.“Ni Ngoma ya kwanza kuiachia kutoka kwenye album yangu ya kwanza kama Zachaa itakayotambulika kwa jina la ‘Mtoto wa Mama’ so hiyo ngoma imebeba jina la Album (Mtoto wa Mama).  Album itakuwa na ngoma 10 na itakuwa sokoni mwezi wa 12  mwaka huu 2014. Lakini hii ngoma itakuwa hewani Jumatatu ya wiki ijayo,” amesema.

No comments:

Post a Comment

paulmkale