Zaidi ya mwezi mmoja uliopita Alikiba alikata kiu ya mashabiki wake waliomiss kazi zake kwa muda mrefu, kwa kuachia nyimbo mbili kwa mpigo ‘Mwana’ na ‘Kimasomaso’, lakini hadi sasa bado hajatoa video.Alikiba ameweka wazi mipango ya kufanya
video ya ‘Mwana’,anatarajia kuanza kushoot mwezi huu (September).“Tulikuwa tuna organize na director tayari tumemaliza kila kitu kwahiyo mipango ni kufanyika tu, mwezi huu inaweza ikatoka”, alisema.
Hata hivyo Alikiba hakuwa tayari kusema video ya ‘Mwana’ ata shoot wapi, “Siwezi kusema itakuwa wapi…” na alipoulizwa kama itakuwa ndani au nje ya Tanzania alijibu, “wala sio Afrika”.
So kwa majibu ya Alikiba, unahisi video ya ‘Mwana’ itafanyika nchi gani nje ya bara la Afrika?
Tufanye kama alivyosema Cindy Rulz ‘Lets Wait’!!
No comments:
Post a Comment
paulmkale