Rapper Roma Mkatoliki, amewatataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya video ya wimbo ‘Maumivu’ aliofanya na Bob Junior.akiwa safarini kuelekea mjini Musoma kwenye Serengeti Fiesta 2014, Roma amesema
yeye na Bob Junior wamekubaliana kutouimba wimbo huo kwenye show zao.
“Tupo speed sana kwenye maandalizi ya video tupo kwenye tour, Bob ana ziara na mimi kama unavyoniona. Sasa hivi tupo mbioni kufanya video ambayo itachukua kama wiki mbili mpaka kukamilika na kuweza kutoka,” amesema Roma.
“Halafu ndo inakuwa full package ya nyimbo kwamba audio ilishatoka pamoja na video. Kutokana na tour ambazo tunazifanya kuna kitu ambacho tumejiwekea mimi na Bob Junior, kwamba hatakiwi kuiperform ile nyimbo kwa sasa na Roma pia hatakiwi kuiperform hiyo nyimbo kwa sasa. Halafu itafikia time tutaanza kuiperform kwa sababu kuna tour zimetuingilia katikati wakati na sisi tunarelease ngoma ikasababisha tutofautiane muda wa kuperform hiyo nyimbo.”
“Hiyo inatusaidia kwa sababu inawapa watu kiu, watu wakiona Roma yupo kwenye Fiesta wanategemea Roma ataimba wimbo wa Maumivu Halafu sasa Roma anakuwa haimbi, halafu itafika time tutaanza kufanya tour kwa sababu ya wimbo Maumivu na tunaamini itafanikiwa baada ya muda fulani,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment
paulmkale