Christian Bella aingiza zaidi ya shilingi milioni 30 kwenye show ya ‘Nani Kama Mama’

Msanii wa muziki wa dansi, Christian Bella anayetamba na kibao chake cha ‘Nani Kama Mama’ amedai kuwa show yake ya ‘Nani kama Mama’ aliyoifanya hivi karibuni imemuingizia zaidi ya shilingi milioni 30.Bella amesema
kutokana na matokeo aliyopata, anajipanga kuzungumza na Ommy Dimpoz ili wafanye tour ya pamoja.

“Kwanza nawashukuru wadau wote pamoja na mashabiki kwa kunifikisha hapa, kwanza kwenye show nilifanya mistake kwa kufanya ile show pale Mzalendo. Pale Mzalendo sio pakufanya ile show, ningefanya sehemu ambayo ingeweza ingiza watu kama elfu tano hivi, ila pale inaingiza watu 1,500, kwahiyo ikafurika baada ya kuingiza watu elfu mbili kwa nguvu na kiingilio kama unavyojua kilikuwa elfu 20,000. Hapakuwa na complementary ni pesa tu,” amesema muimbaji huyo. “Tulipata pesa nyingi, kwahiyo zaidi ya watu kama elfu tatu walibaki nje. Parking ikageuka ikawa ukumbi, cha kushangaza mvua ikawa inanyesha lakini bado watu wakaendelea kula burudani. Kwahiyo watu walishindwa kufurahia kwa sababu watu walikuwa wamebanana sana.”

“Mwisho wa siku watu wameomba turudie tena hiyo show, ndo tunaangalia tunaweza tukachagua tarehe ngapi, pia tunaanza tour hivi karibuni ya kufanya show kama hiyo ya Dar ‘Nani Kama Mama tour, kwahiyo itabidi tukae mimi na Ommy Dimpoz tuangalie tunafanyaje kazi.”

No comments:

Post a Comment

paulmkale