Diamond asema vurugu zilizotokea kwenye show ya Ujerumani ni ‘booster’ kwake

Pamoja na kwamba mapromoter Wanigeria walioandaa show ya Diamond iliyoshindwa kufanyika weekend iliyopita mjini Stuttgart, Ujerumani baada ya kutokea vurugu kubwa, upande wa Diamond Platnumz amesema
kwake haoni kama tukio hilo limemchafua kwa namna yoyote na badala yake anaona limempa ‘kiki’.“Sidhani kwasababu karibuni asilimia tisini walijua nini kinachoendelea hawakujua kabisa tatizo lilikuwa kwa msanii…hiki kitu kiko wazi na hata promota nasikia amezungumza kuwaambia kwamba halikuwa tatizo la msanii” amesema Diamond kupitia 255 ya Clouds Fm.

Diamond amesema kuwa baada ya tukio hilo asubuhi yake vyombo vingi vya habari vya Ujerumani viliandika habari hiyo ambayo kwa upande wake hiyo ni faida.


Uharibifu uliotokana na vurugu hizo

“mi nachokiona sana sana naona busta tu kwasababu asubuhi yake iliandikwa katika blog kibao za Ujerumani magazeti ya Ujerumani, katika vitu viiingi vya Ujerumani viliandika kama ilitokea hivi na hivi na hivi afu kila ikiandikwa itamuandika Diamond wanaweka picha ya Diamond. So kwa namna moja ama nyingine Mwenyezi Mungu alitumia njia ile kufanya watu wa Ujerumani kama kuna mtu anaitwa Diamond wajue kuna mtu anaitwa Diamond”.

Hata hivyo kwa upande mwingine Platnumz amesema alijisikia vibaya pamoja na kwamba alilipwa pesa yote lakini kama msanii kuna kitu muhimu alichokikosa.

 “Kiukweli nilijiskia vibaya kwasababu msanii hakuna kitu unachokifurahia kwanza kama show ijae kwasababu show ikijaa kwanza ni credit, ni cv kubwa sana unajua unavyopost ile picha umejaza unawatengenezea promoters wengine kuona kama huyu mtu anakubalika”.

No comments:

Post a Comment

paulmkale