Pamoja na kuendelea kupata mashabiki wapya kila kukicha vijana wa Mkubwa na Wanawe, Yamoto Band wanatarajia kuachia ablum yao ya kwanza mwaka huu ambayo watashirikisha msanii mmoja wa Kenya na mmoja wa
Nigeria.“Mipango mikubwa iliyopo album ndio kitu cha kwanza, lakini tunataka tutengeneze album ya video na audio kwa wakati mmoja…”
Meneja wa bendi hiyo Said Fella ameiambia Bongo5 kuwa, tayari wamerekodi nyimbo 13 lakini sasa wanaangalia uwezekano wa kuwashirikisha wasanii wa Nigeria na Kenya kwenye album hiyo.
“nyimbo zimeshatimia za album, kuna nyimbo kama 13 ila kuna mmoja tulikuwa tunategemea lazima tutafute mtu kutoka Kenya halafu nyimbo nyingine tunapaswa tutafute mtu kutoka Nigeria ilimradi tuongeze ladha katika hiyo album, kwasababu kwa sasa hivi kwa Tanzania tumeshafanya na Jose Mara na Christian Bella…”
Aliendelea,
“Nigeria hatutaki jina kubwa sana kwasababu ukianza jina kubwa sana nwisho ukitaka kutengeneza ya pili tutakuwa tayari tushamaliza, ndio maana hata hapa Tanzania tulisema kwanza tunaanza na hawa watu hawa afu baadae tufikirie wasanii wakubwa wa Tanzania. Mungu akipenda tutafanya mwaka huu album iishe, ila tukishindwa kupata hao wa West kwa kipindi hiki tukipata tu wa Kenya tunatoa album.”
Fella amesema kutokana na wasambazaji waliopo (wahindi) kusema kuwa kwasasa biashara ni mbaya, wameamua album ya Yamoto itasambazwa mkono kwa mkono.
Mbali na album Fella amesema mradi mwingine unaokuja wa Yamoto ni nguo zao.
“Kingine tunafikiria kuwa na nguo zao, yaani kutengeneza nguo za Yamoto na kuwapelekea mashabiki zetu”.
Wiki hii Yamoto wameachia video ya wimbo wao mpya ‘Niseme’.
No comments:
Post a Comment
paulmkale