Video mpya ya ‘Mr Nay’ imemfanya Nay Wa Mitego kuwa na kazi ya kujibu maswali mengi kutoka kwa watu mbalimbali wanaomuuliza maana ya kile kinaachoonekana kwenye video hiyo. Miongoni mwa maswali hayo tayari ameyatolea majibu, ikiwa ni pamoja na maana ya idea ya video hiyo ambayo
Nay mwenyewe alisema ni wazo tu alilipata lakini hajui ina maana gani.Swali lingine ambalo Nay Wa Mitego amelitolea ufafanuzi ni,”Zile damu, na vitu vingine kama vya kishetani pamoja na namba ninayopenda kuitumia ya #966 ni vitu vinavyofanya nipate sana msg na kuulizwa maswali”, alisema Nay alipozungumza na Millard Ayo.
Kuwaondoa hofu wale walioanza kupata wasiwasi kutokana na video hiyo ikiwa ni pamoja na mama yake mzazi, Nay amesema:
“na ndivyo vitu vimemshtua mama mpaka akaniita, watu wengine wanadhani mimi ni mwabudu shetani ila nataka watu watambue kwamba hakuna kitu kama hicho, ni ubunifu tu”.
Video ya ‘Mr Nay’ imefanyika nchini Kenya na kuongozwa na Kevin Bosco Jnr.
No comments:
Post a Comment
paulmkale