Mwan fa Anatarajia Kuachia Collabo Mpya Ambayo Amemshilikisha Ali Kiba"KIBOKO YANGU"

Kabla ya kuachia ‘Mfalme’ aliyomshirikisha G-Nako, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA alikuwa amepanga kutoa wimbo aliomshirikisha Alikiba, ‘Kiboko Yangu’. Na pia ‘Kiboko Yangu’ ndio wimbo alioanza kurekodi kwenye studio za MJ Records chini ya producer
Marco Chali lakini aliamua kuanza kuachia ‘Mfalme’ iliyotayarishwa na Nahreel.Hata hivyo kwa mujibu wa tweets za Mwana FA na Alikiba, huenda zamu ya kuachiwa wimbo huo umekaribia. Kupitia Twitter, shabiki amemuuliza Alikiba lini wataitoa ngoma hiyo aliyoshirikishwa na Mwana FA na kujibu ‘soon’ huku FA naye akiongezea jibu hilo hilo.

Hivi karibuni FA alitweet:

Hii ngoma yangu na Alikiba inaniwasha,NATAKA kuitoa!!lakini…

— Hamis Mwinjuma (@MwanaFA) August 31, 2014

Kwenye mahojiano aliyoyafanya mwezi May mwaka huu na kituo kimoja cha redio, FA alisema: Watu wengi ambao walikuwa wamezisikia hizi nyimbo mbili mwanzoni walikuwa wameichagua hiyo na Alikiba ndio iende kwanza na mi pia nilifikiri hivyo.

Lakini ngoma na Alikiba iko na tukienda kufanya video ya hii Mfalme nafikiri tuta shoot na hiyo ya Alikiba pia kwa wakati huo huo tuwe nayo tu kwapani, tukijiskia kwamba watu maskio yao yameshachoka kuskia Mfalme wanataka kitu kingine tutawagonga nayo tu, video inaenda kufanyika Nairobi.”

No comments:

Post a Comment

paulmkale