Baba Levo Apata Ajali Akiwa Ndani Ya Basi La Am Lililogongana Na Coaster
Msanii wa kundi la 2mbili wa Town, Baba Levo amepata ajali baada ya basi
la kampuni ya AM Coach alilokuwa amepanda kugongana na Coaster.
Kwa mujibu wa ajali hiyo imetokea kwenye pori la
kijiji cha Uluwila ambapo alikuwa anatokea Tabora kwenda Mpanda.
Inadaiwa kuwa dereva wa Coaster alikuwa akikwepa barabara mbovu na hivyo
kuhamia upande ambao basi la AM lilikuwa likija na hivyo kugongana uso
kwa uso.
Baba Levo amesema ameumia usoni na mwilini kwa kuchanwachanwa na vioo vya mbele vilivyopasuka kwenye basi.
“Ameweza kuona kuna baadhi ya watu wamefariki ambapo kati yao ni
waliopasuka vichwa na shingo,” umeandika mtandao huo. Coaster hiyo
inadaiwa kufumuka upande wake wa juu huku kukiwa bado na abiria
waliobanwa kwenye Coaster hiyo.
No comments:
Post a Comment
paulmkale