Rekodi aliyoivunja Diamond Platnumz na kuiacha ya P Square

Tumeshazoea kuona baadhi ya mastaa wa Afrika wanapoweka video zao kwenye youtube wanapata views nyingi ndani ya siku..> chache lakini Good news time hii imeangukia kwa mkali wa Tanzania.

Mmiliki wa hit single ya ‘Mdogo Mdogo’ Diamond Platnumz ameipiku video ya wakali wa Nigeria P Square baada ya kupata views nyingi ndani ya siku nne.

Video ya P Square  ‘Shekini’  iliyowekwa youtube Nov 17 ina views 286,165 huku Diamond ambaye  video yake ‘Nitampata Wapi’ iliyoweka Nov 20 ina views 354,910.

No comments:

Post a Comment

paulmkale