Ndoa ya Sheta Yafikisha miaka miwili sasa

Shetta na mke wake Leila wametimiza zaidi ya miaka miwili kwenye ndoa yao na rapper huyo amedai kuwa ni furaha tu ndio iliyotawala familia yake.Shetta na Leila walifunga ndoa mwaka 2012 na hadi sasa wamebarikiwa mtoto mmoja wa kike aitwaye Qayllah.

Rapper huyo amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpa nguvu huku familia yake ikiwa ni yenye upendo na amani.

“Mimi nilioa huko nyuma na matunda yake ndo haya unayaona, Qayllah. Nilioa lakini sikufanya sherehe, ilikuwa kimya kimya saa kumi na mbili baada ya watu kumaliza ile swala ya saa 11 ndo ikapita. Kwahiyo Mama Qayllah ni mke wangu wa ndoa. Sikupiga picha wala nini.


Qayllah

“Watu wengi hawakufahamu kwa sababu haikuwa na shamra shamra pia sikupenda kuweka wazi mambo yangu ya kifamilia kwa wakati huo. Lakini namshukuru Mungu mpaka sasa hivi nafurahia maisha yangu pamoja na familia yangu,” aliongeza Shetta.

No comments:

Post a Comment

paulmkale