Klabu ya Simba ya jijini Dar-es-salaam iko mbioni kuingia mkataba ba
kocha mpya kutoka Serbia baada ya kumalizana na kocha Mzambia Patrick
Phiri ambaye alifukuzwa kazi siku chache zilizopita .
Kocha huyo Goran Kapunovic aliingia nchini Tanzania akitua kwenye
uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere hapo jana saa 1
asubuhi na alikuja kupokewa na viongozi wa Simba akiwemo mjumbe wa timu
hiyo Colin Firsch .
Simba ilimfukuza Phiri mapema wiki hii baada ya klabu hiyo
kutoridhika na kiwango cha timu hiyo kufuatia mfululizo wa matokeo
mabaya hasa kwenye mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambapo
wekundu wa msimbazi walifungwa 1-0 .
Moja ya vichwa vya habari vya magazeti ya michezo hapa nchini ambavyo vimebeba ‘story’ kuhusu kocha mpya wa Simba.
Simba kwa sasa iko visiwani Zanzibar ambako inashiriki michuano ya
kombe la mapinduzi huku ikiwa chini ya kocha msaidizi wa timu hiyo
Suleiman Matola ambaye ataiongoza timu hiyo hadi hapo kocha mpya
atakapoungana rasmi na kikosi chao.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichomo ndani ya klabu hiyo ambacho
hakikuwa tayari kunukuliwa Phiri tayari ameagana na wachezaji wa timu
hiyo baada ya maamuzi ya kuachana nae .

Goran
Kopunovic (wa pili upande wa kushoto kwenye mstari wa mwisho) akiwa na
kikosi cha klabu ya Ferencvaros ya nchini Hungary kwenye msimu wa mwaka
1995/96.
Kocha huyo mpya ni raia wa Serbia na aliwahi kucheza kwenye michuano
mikubwa ya ligi ya mabingwa barani ulaya akiwa na timu ya Ferencvaros ya
nchini Hungary na mara ya mwisho alikuwa anafundisha klabu ya Polisi ya
huko Rwanda .
Simba itaingia uwanjani usiku wa leo kucheza mechi yake ya kwanza ya
kombe la mapinduzi dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Amaan
visiwani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
paulmkale