Vanessa Mdee athibitisha uhusiano na Jux kwa picha hii?
Kwa mara kibao Vanessa Mdee na Jux wamekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi licha ya kuonesha dalili nyingi ya kuwa ni item.
A picture is worth a thousand words
Lakini huenda mastaa hao wanataka kuufanya uhusiano wao official kwa
mwaka 2015. Vee Money ametoa hint kuhusu uwezekano wa wawili hao kuwa
pamoja kwenye picha aliyoweka Instagram leo.
“A1 since Day 1,” ameandika Vanessa kwenye picha hiyo ya black and white
inayoonesha wazi kuwa wapo kwenye dimbwi la mahaba mazito.
Akijibu swali la kama ana uhusiano wa kimahaba na muimbaji huyo wa
‘Nitasubiri’, Vanessa aliwahi kujibu,”Unajua labda watu hawafahamu tu
lakini mie na Jux tumefahamiana muda sana na ni mtu ambaye huwa
tunashauriana hasa mambo ya kazi zetu.”
“Ni rafiki yangu wa muda sana sasa hivi. Unajua watu wakikuona upo na
mtu karibu tu lazima watasema. Mwanzo walisema Ommy Dimpoz sababu ya
ile nyimbo ya Me and You. Mara wakasema Gosby kipindi kile ilipotoka ile
nyimbo ya Monefere. Kwahiyo kwahiyo hata leo mfano Nahareel asingekuwa
na Aika basi nahisi na yeye pia wangesema hivyo. Ila sio hivyo
wanavyofikiria. Jux ni rafiki yangu tu,” Vee
Naye Jux alikuwa na majibu yale yale pindi swali hilo lilipokuwa
likitupwa kwake. “No ni mshikhaji wangu tu, tunafanya naye kazi, kuna
tabia zinaendana, kama ninavyokuwa na rafiki na Stamina, Mo Music ni
kawaida, sema unajua ni mwanamke na ni njia toafuti ndio maana imekuwa
hivyo,” alisema Jux.
Hata hivyo alipoulizwa kama Vanessa anafaa kuwa wife material Jux alijibu Vanessa ana kila sifa ya kuwa mke.
“Ni msichana mzuri, mwonekano wake mzuri, she is smart, yeah she is a
wife material, yuko vizuri, lakini na mimi tumeendana sana tabia zetu
kama washikaji. Sema nipo naye karibu na kwa sababu mimi sionekanagi na
wasichana wengi ndio maana imekuwa hivyo. Lakini sijui labda baadaye kwa
sasa hivi ni mapema, vyote anapanga Mungu,” alisisitiza Jux.
No comments:
Post a Comment
paulmkale