Yamoto Band yauanza mwaka mpya na mashavu ya kimataifa, kwenda Uingereza mwezi wa pili
Bendi ya vijana wadogo inayokua kwa kasi kubwa Yamoto Band, imeuanza
vizuri mwaka mpya kwa kupata show za kimataifa ikiwa ni mwaka mmoja tu
toka itambulishwe rasmi.
Meneja wa Yamoto, Said Fella ametoa ratiba ya bendi hiyo kwa mwaka
huu (2015) , na miongoni mwa show wanazotarajia kufanya miezi ya
mwanzoni ni pamoja na show ya Uingereza.
Kupitia Instagram Fella aliandika:
“Aya wadau napenda ya kuwafamisha ratiba ya mwaka huu ya moto
band leo tar 1 leo daimond kawaalika rwanda tar 4 tupo maisha club
kuzindua ngoma interview tar 10 tupo kigoma tar 31 watawasindikiza
wakubwa zao mh temba, chege na madee kwenye utambulisho wa ngoma na
video walofanya kaburu ukumbi wa escape 1 na tar 14 mwezi wa 2
watakuwepo musoma na tar 21 ndio MUNGU akipenda vijana watakuwa UK
inshaallah MUNGU akipenda”.
No comments:
Post a Comment
paulmkale